» » Jeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-Shabab

Jeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-Shabab


Jeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-shababHaki miliki ya pichaKENYA GOVERNMENT
Image captionJeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-shabab
Wanajeshi wa Kenya wameripotiwa kuwaua wanamgambo 31 wa al-Shabab, baada ya kushambulia kambi yao eneo la Badhade kusini mwa Somalia.
Kwa mujibu na taarifa iliyotolewa na serikali, wanajeshi wa Kenya walitwaa bundiki 11 aina ya AK-47, vifaa vya mawasiliano, chakula na sare za kijeshi.
Uvamizi huo wa siku ya Jumapili ulifanya na vikosi vya nchi kavu vikisaidiwa na helkopta za jeshi.
Serikali ilichapisha picha za badhi ya silaha jeshi lilitwaa ikiwemo milipuko ya kujitengenezea.
Baadhi ya vilupuzi vilivyotwaliwa kutoka kwa al-shababHaki miliki ya pichaKENYA GOVERNMENT
Image captionBaadhi ya vilupuzi vilivyotwaliwa kutoka kwa al-shabab
Kenya kwanza ilipeleka wanajeshi nchini Somalia mwezi Oktoba mwaka 2011 katika kile kilichojulikana kama Oparesheni Linda Nchi, kabla ya kujiunga na kikosi cha Muungano wa Afrika kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Somalia mwaka uliofuatia.
"Tulisikia sauti za ndege zikishambulia sehemu ya Badhade, lakini hatujui hasara iliyotokana na shambulio hilo. Sijui ni kitu gani wanajeshi wa Kenya wanatuhumu kuona katika eneo hilo na hali hawakutujulisha chochote kuhusiana na mashambulizi hayo." alisema mkuu wa wilaya ya Badhade Farah Heibe.
"Igekuwa bora kama wangefahamisha jeshi la Somalia na wakuu wa utawala kuhusu shambulio hilo. Siyo jambo la busara kushambulia maeneo yetu bila ya kuwasiliana nasi, kama nchi huru."
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...