KESHA LA ASUBUHI
JUMANNE-MARCH 07, 2017
FAMILIA KATIKA MGOGORO
"Ndugu zake wakaona ya kuwá baba yao anampenda kuliko Ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani." Mwanzo 37:4.
▶Dhambi ya Yakobo na msururu wa matukio ambayo dhambi hii iliuleta, havikushindwa kuweka mvuto wa uovu -mvuto ambao ulidhihirisha matokeo yake machungu kwenye kwenye tabia na maisha ya wana wake. Hawa vijana walipofikia hatua ya kupevuka, wakaendekeza makosa mazito, matokeo ya mitala yakadhihirika pale nyumbani. Uovu huu wa kutisha huwa unakausha chemchemi halisi za upendo na mvuto wake unadhoofisha vifungo vilivyo vitakatifu sana.Wivu wa wanawake ulikua umeweka umeweka machungu kwenye uhusiano wa kifamilia, watoto wakawa wagonvi na wasioweza kujitawala na maisha ya baba yakatiwa giza kwa fadhaa na huzuni.
▶Hata hivyo, alikuwapo mmoja mwenye tabia tofauti kabisa -Yusufu,mwana mkubwa wa Raheli, ambaye uzuri wake haukuwa wa kawaida ulionekana kuakisi uzuri wa ndani wa akili na moyo. kijana kijana huyu alikuwa msafi ,mtendaji wa mambo na mwenye furaha,alidhibitisha ukweli wa maadili na uthabiti.Alisikiliza maelekezo ya baba yake na alipenda kumtii Mungu...Kwa sababu mama yake alikuwa amekufa ,upendo wake ulimfungamanisha kwa karibu zaidi na baba yake namoyo wa Yakobo ukafungamana na mtoto wake huyu wa uzeeni."Akampenda Yusufu kuliko wanawe wote."
▶Lakini,hata kupenda huko baadae kungelikua ni sababu ya matatizo na huzuni. Bila kutumia busara,Yakobo alidhihirisha hali yake ya kumpenda zaidi Yusufu na hivyo akaibua wivu wa wanawe wengine....Zawadi ya baba ambayo ambayo haikutolewa kwa busara kwa Yusufu ,ya kanzu nzuri ndefu, ....iliibua mashaka kwamba alikuwa amekusudia kuwaruka wanawe waliokuwa wakubwa na kumpa haki ya uzaliwa wa kwanza mwana huyu wa Raheli.Kijicho chao kiliongezwa zaidi pale kijana alipowaambia siku moja siku moja juu ya ndoto aliyokuwa ameiota....
▶Kijana aliposimama mbele ya kaka zake, mwonekano wake mzuri wa uso uling'azwa na roho mwenye kuvuvia, hawakuweza kujizuia kuvutiwa kwao; lakini hawakuona ni bora kuacha njia zao mbaya na wakachukia usafi ule ambao ulikua kemeo kwa dhambi zao. Roho ile ile iliyomsukuma Kaini ilikuwa ikiwaka mioyoni mwao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment