Wenye Thamani Zaidi
Akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Waebrania 11:26.
Musa alikuwa mwanafunzi. Alielimika vizuri katika elimu yote ya Wamisri, lakini hii haikuwa sifa pekee aliyohitaji katika kumuandaa kwa ajili ya kazi yake. Kutokana na majaliwa ya Mungu, ilimpasa ajifunze kuwa na subira, kuzuia shauku zake. Katika shule ya kujikana nafsi na matatizo alikuwa apate elimu ambayo ingekuwa ya muhimu sana kwake. Majaribio haya yangemwandaa kuonesha uangalizi kama baba kwa wote ambao wangehitaji msaada wake. Hakuna ujuzi, hakuna elimu, hakuna ujuzi wa kujieleza ambao ungeweza kusimama badala ya uzoefu huu katika majaribio kwa mtu ambaye alikuwa achunge roho ambazo zitawajibika kutoa hesabu baadaye. Katika kuifanya kazi ya mchungaji mnyenyekevu, katika kusahau nafsi na kupendezwa na kundi alilokabidhiwa kulichunga, ilibidi aandaliwe kwa ajili ya kazi iliyotukuka sana ambayo imepata kukabidhiwa kwa watu, ile ya kuwa mchungaji wa kondoo wa malisho ya Bwana.
Wale wanaomcha Mungu duniani lazima waunganishwe naye. Kristo ni muelimishaji mkamilifu ambaye dunia haijapata kuona. Kupokea hekima na ujuzi kutoka kwake kulikuwa kwa thamani kwa Musa kuliko elimu yote ya Wamisri….
Imani ya Musa ilimuongoza kuangalia mambo ambayo hayaonekani, yale ya milele. Aliacha mivuto ya fahari ya maisha ya ikulu kwa sababu dhambi ilikuwa pale. Aliacha mambo ya wakati uliopo na yaliyoonekana kuwa mazuri ambayo yalidanganya na kufikisha hatua ya kuharibu na kuangamiza. Mivuto ya kweli, ya milele, ilikuwa ya thamani kwake. Kujinyima kwa Musa kwa kweli hakukuwa kujinyima. Kwake yeye ilikuwa ni kuacha mambo ya wakati huu, yanayoonekana, yenye uzuri unaoghilibu, kwa ajili ya yale yaliyo ya uhakika, ya juu, yenye uzuri usiokoma.
Musa alistahimili shutuma za Kristo, akiona shutuma kuwa utajiri mkubwa kuliko hazina zote za Misri. Aliamini kile ambacho Mungu alisema na hakuvutiwa kuyumba kutoka katika uadilifu kutokana na shutuma zozote za kidunia. Alipita katika dunia kama mtu huru wa Mungu… Aliangalia vile visivyoonekana na hakusita. Fidia ya tuzo ilimvutia na inaweza kuwa hivyo kwetu pia. Yeye alimfahamu Mungu.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
KESHA LA ASUBUHI
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment