» » Dkt Mohamed Shein achukizwa na vitisho vya Tanesco

Dkt Mohamed Shein achukizwa na vitisho vya Tanesco

Image captionRais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein asema hatishwi na vitisho vya Tanesco

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wala jana.

Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco kutoa ilani ya siku 14 kwa wadeni wake kwamba litawakatia moto.

Hatua hiyo ya Tanesco inajiri baada ya rais Magufuli kuiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadeni wake wote kikiwemo kisiwa cha Zanzibar.

Tanesco kuwakatia umeme walio na madeni TanzaniaMagufuli aagiza Tanesco kuwakatia umeme wasiolipa TanzaniaUmeme wakatika ghafla Tanzania

Makamu wa rais wa kwanza nchini Tanzania Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia.

Ziara hiyo ya Indonesia ilikuwa ya kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi ambapo alimwakilisha Rais John Magufuli.

Amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yoyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein ameelezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema utaleta tija na faida kubwa kwa Wazanzibari na Watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii, uvuvi, ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...