MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
MAFUNGU: Walawi 11; Kumbukumbu ya torati14; Walawi 7:22-24;
“Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31).
“Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31).
Sokwe hajawahi kubadili mfumo wake wa kula,lakini mwanadamu mwenye akili timamu amepotea kabisa.
Mungu hajakunyima chakula,chakula kipo,ametupa maelekezo bora ya kutunza afya zetu kwa kanuni ya vyakula bora kiafya na namna mtindo wa maisha wapaswa uwe. Vyakula anavyotuambia kuwa tunaruhusiwa kuvila ni vyema sana kwetu na vinatusaidia katika ukuaji wa kiroho na kimwili. Vyakula anavyotuambia tusivile vinatufanya kushambuliwe na magonjwa.

Biblia katika Kumbukumbu la Torati 14 Mambo ya Walawi 11 ina orodha ya ndege, wanyama, na samaki ambao Mungu alisema hawafai kuliwa. Kwa mujibu wa sura hizo, wanyama safi ni lazima kwato zao zigawanyike na pia wacheue. Samaki safi ni lazima wawe na magamba na mapezi, vyote viwili. Ndege wanaokula uchafu,nguruwe,sungura,wibari, samaki wakiwemo papa,katfish, nyangumi, pomboo, dagaa kamba, kaa, kambakoche, chaza mdogo, chaza mkubwa, na wengine wengi ni najisi,haramu ni machukizo kwa Mungu.
Watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tena wanaishi kwa muda mrefu zaidi.Wataalamu wengi wa mambo ya afya na lishe wanatushauri kutumia chakula kile cha awali walichopewa wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mbogamboga kwaajili ya ustawi wa afya zetu. Wanadamu katika matumizi mabaya ya biblia Marko7:14-15, 18-21, ndani ya moyo hutoka mawazo machafu. Biblia katika Mwanzo 9:4 “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.”
Thamani ya mwili wako haifananishwi na kitu chochote,tutunze miili yetu.Tusiingize taka katika miili yetu,fedha na mali ulizonazo hazina thamani kulinganisha na mwili ulioumbwa na Mungu kwa mfano wake.Mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu tumeagizwa tuutunze.Masikio urembo husikia chochote.
Mtu muadilifu huisikia sauti ya Mungu na kumfuate popote aendako. Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.Amen

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment