» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: MAOMBI YA DAUDI

USHINDI HATIMAYE- MAOMBI YA DAUDI

MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza

Mafungu: 1 Samwel 17:45, 46; Matend13:22,Yakob 4:3;Zabur 86:1-8;Yoh 16:11

“….akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote”. (Matendo 13:22)

Daudi ni shujaa wa imani na mfano wa kuigwa katika safari ya imani.Daudi alikuwa mtu ambaye aliheshimiwa na watu wake sana. Yeye alikuwa kiongozi mashuhuri sana.Wakati anapeleka maombi yake kwa Mungu, hakwenda kama mfalme bali alikuwa kama mtumishi ambaye alimtegemea Mungu kwa kila jambo. Kwa unyenyekevu wake Mbingu zinashuhudia kwamba likubalika machoni pa Mungu.

Daudi alijifunza kumtegemea Mungu nyakati zote na hivyo kuzungumza na Mungu kwake halikuwa ni jambo la kupanga ratiba.Bila kujali kulikuwa na nyakati za kuanguka lakini alimkumbuka Mungu na kumlilia.Ukiporomoka usibaki kwenye maporomoko,nyanyuka songa mbele Bwana yu akushindia vita.
Watu wengi maombi yao hayajibiwi ni kwasababu wanaomba ili wajulikane na watu.Wengine wanaomba huku wakiwa na miungu katika miili yao na kwenye majumba yao.Hata wengine wanadiriki kusema jisaidie ndipo Mungu atakusaidia.Mwambie Mungu akufundishe unyenyekevu,nanda kwake ukijua ya kwamba ni mwingi wa rehema na halinganishwi na kitu chochote.Mungu ni mkweli na mwaminifu hujibu maombi.

Tunaomba vibaya kama Biblia katika kitabu cha Yakobo 4:3,Mungu anapokupatia mafanikio si kwaajili yako binafsi,anakuta uwa mbaraka kwa wengine.Tunapokuwa na kiburi Mungu hawezi kujibu maombi yetu,mwombe Mungu akupe moyo wa unyenyekevu ndani yako.Omba kulingana na mapenzi ya Mungu ndani yako ,mtukuze Mungu katika maombi yako USHINDI NI HAKIKA.

Siri ya kujibiwa kwa maombi ya Daudi ilikuwa,kwanza  alidharau silaha zote za dunia, mbele ya Mungu aliye hai mtangazie shetani kwamba silaha zake zote ni bure. Silaha yake aliitaja kwa adui kwamba ilikuwa JINA LA BWANA NA MUNGU WA MAJESHI,jina la BWANA lina nguvu kushinda majina yote.Alimwambia adui jinsi BWANA WA MAJESHI ATAKAVYOPIGANA VITA kwaajili yake.Mpende mtoa mafanikio hata mafanikio yakitoweka mtoa mafanikio aishi milele zote. Siri nyingine ya ushindi wa Daudi ni kwamba alitaja LENGO LA USHINDI wake. (1Samwel 17:45, 46).AMEN

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...