» » Changamoto za ziwa Victoria kutatuliwa

Changamoto za ziwa Victoria kutatuliwa



TanzaniaHaki miliki ya pichaVICE PRESIDENTS OFFICE
Image captionwaziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustin Mahiga,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan na kulia ni waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan, amewataka wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan, ametoa kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa siku Mbili unaojuisha wadau wa mazingira, wanasayansi na watafiti wa bonde la Ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua mbinu mpya na bora za kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika Bonde la Ziwa Victoria.
Amehimiza kuwa kutokana na muhimu wa bonde hilo ni vyema wadau wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kujumuika pamoja katika kulinda na kuendeleza uhifadhi wa bonde hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema bonde la Ziwa Victoria bado linakabiliwa na changamoto nyingi hasa kuibuka tena kwa magugumaji ambayo yameathiri shughuli za uvuvi, usafiri na kuchafua maji katika Ziwa hilo hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwemo wanasayansi na watafiti kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo ambazo ni tishio kwa uhai wa Ziwa Victoria.
"Kufanya Maamuzi kwa kuzingatia ushauri wa kisayansi ni jambo zuri na la msingi katika kutunga sera ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda na kuhifadhi Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote"amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza anaimani kubwa kuwa majadiliano yatakayofanyika katika mkutano huo yatakuja na mbinu mpya ambazo zitatumika katika kuhifadhi na kuendelea Bonde la Ziwa Victoria.
Katika Mkutano huo wa siku Mbili unaofanyika Jijini Mwanza jumla ya mada 44 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na wadau wa mazingira, wanasayansi na watafiti.
Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya hoteli ya Malaika uliyopo Jijini Mwanza.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...