» » WASANII Wanaosambaza Ujumbe wa Matumizi ya Mihadarati Kusakwa

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo Msikhela amedai wamejipanga kufanya msako dhidi ya wasanii wanaosambaza ujumbe wa matumizi ya mihadarati.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Kamishna huyo alisema hivi sasa wapo kwenye msako dhidi ya wasanii ambao wamekuwa wakisambaza ujumbe wa matumizi ya mihadarati hiyo kwa kuwa wasanii hao ambao ndio kioo cha jamii, sasa wamekuwa wa kwanza katika kusambaza ujumbe wa matumizi hayo.

“Mimi binafsi simfahamu Chid Benz kama ni mtu maarufu aliyekuwa akifahamika kwa kiasi hicho, lakini baada ya kumuona kwenye mitandao ya kijamii ndipo nikaanza kumfuatilia,” alisema Kamishna Msikhela.

Alisema endapo wakipata taarifa ya kwamba wanatumia hadharani na kuwakamata, basi watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine.

“Hawa wasanii tunawasaka nao watuhumiwe kama wahalifu wengine na wakichukuliwa hatua itakuwa fundisho kubwa kwa vijana ambao walikuwa na nia ya kujiingiza katika mtandao huo,’’ alisema.

Alisema ni vema kwa vijana wasiwafuate watu maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wanaushawishi mkubwa kiasi katika matumizi ya dawa hizo.

Kamishna Msikhela alisema wimbi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 30 ndilo ambalo linajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.

“Vijana hawa ndio ambao wangekuwa tegemeo, vijana wa umri huo ndio ambao wangekuja kuwa viongozi wa baadaye, yaani kwa umri huo ndiyo wanaandaliwa kuwa madereva, mawaziri, wakulima, lakini leo wanakuwa mateja, ni jambo la hatari sana,’’ alisema.

Kamishna Msikhela alisema Jeshi la Polisi kwa sasa liko katika mkakati maalumu wa kuhakikisha elimu katika jamii inatolewa ili wananchi waweze kuelimika.

Alisema ulimaji wa bangi mashambani ni mkubwa kuliko mirungi, lakini aliongeza kuwa kama mateja mitaani wanapungua basi hata uingizaji wa dawa hizo kwa sasa nao umepungua.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...