» »Unlabelled » Siri za ndoa

*JE,WAZIJUA SIRI KUMI ZA NDOA*

1. *KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAE ANA UDHAIFU WAKE*
*Mungu* pekee ndio haana udhaifu, Kila ua waridi lina chimbuko lake.

2. *KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAE ANA HISTORIA YAKE MBAYA*
Hakuna mtu ambae ni malaika,epuka kuchunguza mambo ya mtu ya nyuma samehe na usahau.

3. *KILA NDOA INA CHANGAMOTO ZAKE*
Ndoa sio kitanda cha maua waridi yanayomeremeta kila muda,kila ndoa yenye mafanikio imepitia misukosuko mingi.

4. *KILA NDOA INA HATUA ZAKE KATIKA MAFANIKIO*
Hatuwezi kuwa sawa, kuna watakaokuwa mbele kidogo na watakaokuwa nyuma kidogo. Kupunguza stress, kuwa mtulivu, fanya kazi kwa bidii na kwa muda muafaka ndoto za ndoa yako zitatimia.

5. *KUOA AU KUOLEWA NI KUTANGAZA VITA*
Ukishaoa au kuolewa ni kuingia katika uwanja wa mapambano,Kuwa tayari kupambana kuulinda ukanda wa ndoa yako.

6. *HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA*
Hakuna ndoa ambayo imetimilika,Ndoa ni kazi ngumu,jitolee mwenyewe na ufanye kazi ya kuijenga ndoa yako iwe kamilifu.

7. *MUNGU HAWEZI KUKUPA MTU KAMILI UNAYEMTAKA*
Mungu atakupa mtu ili wewe umtengeneze jinsi wewe unavyohitaji yeye awe.

8. *KUOA NI KUJIINGIZA KATIKA HATARI*
Huwezi jua nini kitatokea baada ya ndoa, hali inaweza badilika,hivyo achia nafasi ya marekebisho.

9. *NDOA SIO MKATABA WA MUDA BALI NI MKATABA WA KUDUMU*
Ndoa inahitaji ahadi ya kudumu,mapenzi ni gundi ambayo huwafanya wanandoa kuwa pamoja daima..Talaka huanza katika mawazo.

10. *KILA NDOA HUHITAJI KUJITOA*
Hakuna mapenzi rahisi katika ndoa,huwezi kupenda au kupendwa bila kujitoa nafsi yako kwa dhati.

*Vijana karibuni sana katika familia za wanandoa ila unatakiwa utoe uoga*

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...