Macho na masikio ya mashabiki wa soka Afrika, yataelekezwa nchini Gabon kuanzia Januari 14 katika Fainali za Mataifa ya Afrika.
Jumla ya timu za mataifa 16 zitapambana kutafuta bingwa wa Afrika mwaka huu. Wachezaji mbalimbali wa Kiafrika, wamemiminika nchini humo kutoka kona zote za dunia kwa ajili ya michuano hiyo. Wapo wanaocheza Ligi Kuu ya England, Hispania, Italia, Ufaransa na nyingine nyingi.
Kuna wachezaji waliotoka bara la Asia wakicheza soka la kulipwa huko, lakini wengine hapa hapa Afrika. Ingawa Tanzania haishiriki michuano hiyo, lakini Ligi Kuu Tanzania Bara haipo nyuma kutoa wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya AFCON. Wachezaji hao ni wale waliochaguliwa na mataifa yao waliofuzu kwenda kuzitumikia nchini zao.
1. Juuko Murshid-Uganda (Simba)
Beki huyu wa kati wa klabu ya Simba atakuwa ni mmoja wa wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo, kutoka kwenye Ligi Kuu ya Tanzania.
Ni mchezaji aliyepenya kwenye mchujo wa kocha wa timu hiyo, Micho. Ni mmoja wa mabeki ambao wameisaidia sana Uganda Cranes kutinga hatua hiyo, kwani alikuwa akiitwa na kucheza mechi zote kwenye ngazi ya makundi.
Ni beki mwenye sura mbili. Akiwa kwenye Ligi Kuu Bara, anatajwa kuwa ni beki anayecheza kibabe zaidi na kuogopewa na mastraika wengi.
Hata hivyo, huwezi kudhani kama ni yeye, akiwa kwenye timu yake ya taifa kwa jinsi anavyocheza kistaarabu zaidi.
Staili zote mbili, humfanya kuwa beki mwenye uwezo mkubwa na kikwazo kwa mastraika.
Beki huyo mwenye miaka 26, alisajiliwa na Simba miaka mitatu iliyopita na kati ya wachezaji watatu wa Ligi Kuu Tanzania yeye ndiye ananafasi kubwa zaidi ya kucheza mechi za AFCON kwani ni mhimili katika safu y ulinzi ya Uganda.
2. Vicent Bossou-Toto (Yanga)
Bossou akimkaba Didier Drogba wakati wa Fainali za AFCON mwaka 2013.
Mwingine anayecheza soka nchini Tanzania na amekwenda AFCON ni Vocent Bossou. Huyu pia ni beki wa kati kama ilivyo kwa Juuko Murshid. Lakini anaichezea Yanga ambao ni mahasimu wakubwa wa Simba, timu ya Juuko.
Amechaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo.
Bossou, ni beki anayemaliza msimu wa pili sasa kwenye klabu ya Yanga, lakini awali alikuwa hakubaliki. Mechi za mwanzo alionekana mzito na mashabiki hawakusita kumwita garasa.
Hata hivyo alianza kubadilika pole pole na kuondokea kuwa beki mhimili mkubwa wa Yanga, hasa baada ya beki aliyekuwa tegemeo kwa wakati huo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa majeruhi.
Hadi leo ndiye beki wa kati tegemeo kwa Yanga. Hata hivyo kuna wasiwasi kama anaweza kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kama ambavyo mwenzake Juuko kwenye kikosi cha Uganda. Hii ni kutokana na timu hiyo kuwa na mabeki wengi kutoka nje ya bara la Afrika, wanaochezea klabu kubwa Ulaya.
3. Bruce Kangwa-Zimbabwe (Azam)
Bruce Kangwa akiwajibika uwanjani
Ni winga wa kushoto wa klabu ya Azam FC. Huyu naye atakuwepo nchini Gabon akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe.
Ni mmoja wa wachezaji walioitoa kimasomaso Ligi ya Tanzania nayo kutoa wachezaji ambao wameitwa na timu zao za taifa na kwenda AFCON.
Hata hivyo, wenyewe Wazimbabwe wamemwita kama beki wa kushoto na si winga, ingawa wanaweza kumtumia vyovyote vile watakavyoona inafaa.
Kangwa ni mchezaji ambaye alisajiliwa msimu huu na Azam FC, na ni mmoja wa wachezaji wa kigeni ambao angalau wanaonekana kuisaidia timu hiyo kwa sasa.
Kama ilivyo kwa Bossou hana nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi cha kwanza japokuwa anaweza kupewa nafasi ya
Uwezekano wa Juuko, Bossou na Kangwa kucheza mechi za AFCON
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment