Klabu ya Yanga inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na kocha wao wa zamani Charles Boniface Mkwasa kwa ajili ya kumrudisha kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeiambia shaffihdauda.co.tz kuwa, kuna uwezekano mkubwa Mkwasa akarejea kwenye benchi la ufundi la Yanga.
“Uongozi wa Yanga tayari umeanza mazungumzo na Mkwasa kwa ajili ya kumrudisha kwenye benchi la ufundi baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.”
Mkwasa ambaye aliondoka Yanga akiwa kocha msaidizi wa Hans van Pluijm kwenda kuifundisha Taifa Stars, baada ya TFF kumfukuza aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mart Nooij.
Juma lililopita TFF ilitangaza kuachana na Mkwasa baada ya pande mbili kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba, swali linalobaki ni kwamba, Mkwasa akirudi Yanga ndio mwisho wa Mwambusi?
Umeisikia hii kuhusu Mkwasa na Yanga
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment