TP Mazembe imefanikiwa kumrudisha kundini nyota wake wa zamani, Tresor Mputu baada ya kushinda kesi dhidi ya klabu ya Kabuscorp ya Angola.
Mputu alishindwa kucheza kwa muda mrefu baada ya kuondoka Kabuscorp ambayo ilidai amevunja mkataba.
Baada ya juhudi kubwa za rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi ambaye alituma wawakilishi wake FIFA,Mputu ameishinda kesi hio na Kabuscorp wameamuliwa kuwalipa TP Mazembe dola milioni 1.5 iliyokuwa ada ya uhamisho wake.
FIFA imeliarifu shirikisho la mpira la JK Kongo, FECOFA kumuidhinisha Mputu kuichezea TP Mazembe kwa mara nyingine.
Mputu anakumbukwa na wengi kwa kuiongoza TP Mazembe kuwa klabu ya kwanza Afrika kufika fainali za Klabu Bingwa Duniani mwaka 2010 walipofungwa na Inter Milan.
Kwa upande mwingine, TP Mazembe imewaongezea mikataba nyota wake, Jonathan Bolingi na Rainford Kalaba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment