» » Sababu za wasanii waliopotea kushindwa kurudi kwenye ‘game’

Sababu za wasanii waliopotea kushindwa kurudi kwenye ‘game’


Kuhusu kufulia na kupotea kabisa kwenye ‘game’ kwa wasanii waliowahi kutamba siyo habari mpya tena.
Taarifa hizi zimekuwa za kawaida sana, hazishangazi wala kustaajiabisha kwa sababu baadhi yao tunaendelea kuwaona na kusikia kila anguko la kuhuzunisha wanalopitia.
Kuna wakati  ilikuwa ukitaka kuizungumzia muziki wa Bongo Fleva mbele za watu na wakakuelewa ni lazima umtaje Chid Benz, Q Chief, Dudu Baya, Ray C, Mike Tee nawengine, lakini leo hii sauti za wasanii hao zinaishi mbali kabisa na masikio ya mashabiki.
Wengine wanaweza kurudia nafasi zao katika chati ya muziki, lakini siyo rahisi kwa msanii kurudi kwenye nafasi yake aliyoipoteza. Yote kwa yote ugumu huo hauji bure, una sababu zake za msingi ambazo ni hizi hapa;
Aina ya wasanii waliochukua nafasi
Msanii anapopotea siyo kwamba anaondoka na tasnia nzima ya muziki, hilo huwa ni tatizo lake binafsi. Muziki huendelea kuishi na kuzalisha wasanii wapya wenye uwezo kama wake au zaidi.
Hivyo wakati msanii anajipanga kurudi hukutana na kikwazo kikubwa cha msanii mwingine ambaye tayari ameshachukua nafasi yake kwa mashabiki.
Ray C na Recho wanaweza kuwa mfano katika hili. Wakati Ray C amepotea, Recho akaibuka na kufanya sawa na Kiuno Bila Mfupa na akabamba kweli kweli.
Wanaimba muziki wa zamani
Idadi kubwa ya wasanii waliopotea wanashindwa kurudi kwa sababu ya muziki wanaoufanya ni wa kizamani ambao hauna nafasi tena kwa vizazi vya sasa.
Unakuta msanii amepotea kwa miaka kumi, lakini anapoanzisha harakati zake za kurudi bado anafanya muziki wa aina ile ile aliyouimba miaka kumi kabla hajapotea
Abby Skillz ni mfano tosha juu ya hili, anajitahidi kufanya muziki lakini bado anaimba kama alivyoimba kwenye wimbo wake  Maria ulitamba sana mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Uhusiano mbovu na wasanii wapya
Wasanii wengi waliopotea huwa na malalamiko yasiyo ya msingi dhidi ya wasanii wapya. Wenyewe huwatazama kama maadui, jambo ambalo hufifisha uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano mzuri miongoni mwao, uhusiano unaoweza kutumika kama ngazi ya kumrudisha msanii kwenye chati kwa sababu mbinu za muziki wa sasa wanazijua wasanii wapya.
Q Chief aliwahi kumtuhumu Diamond kwenye vyombo vya habari kwamba anamroga na kwamba kurogwa huko ndiyo kulikuwa sababu ya kukwama kwake kile alipojaribu kurudi kwenye game.
Msanii Dully sykes yeye anaboresha uhusiano na wasanii na kuendelea kubamba kwenye game kila anapohitaji kufanya hivyo.
Muda wao umekwisha
Kabla ya mimi (mwandishi wa makala hii) kuandika katika huu ukurasa alikuwepo mtu alifanya hivi miaka mingi huko nyuma, lakini kwa sasa muda wake umekwisha, ameweka kalamu chini anafanya mambo mengine; na mimi itakuwa vivyo hivyo pia utakapofika wakati wangu. Hata katika muziki suala hili la wakati lina nafasi yake, hakuna msanii atakayebamba kwa kipindi chote hata kama atapewa umri mrefu kiasi gani.
Kuna wakati utafika mashabiki watachoka sauti na kila kitu chake na hapo watageuzia masikio yao kwa wasanii wengine. Yeye atabaki kuwa ‘legend’ ikibidi.
Unapofika wakati huu msanii hana namna ya kufanya ili kurudi kwenye chati, labda tu aendelee kuimba kwa kujistarehesha.
Kutumia kila ushauri wanaopewa
Bila shaka hili husukumwa na kiu yao ya kutaka kurudi pale walipokuwa awali kiasi kwamba wasanii waliopotea huondosha chujio la ushauri lililopo vichwani mwao na kupelekea kutumia kila ushauri wanaopewa na Prodyuza, msanii mwenzie au mtu yeyote yule wanayemwamini.
Hapa sasa ndio unakuta zamani msanii alikuwa anarap lakini katika harakati zake za  kuhakikisha anarejea kwenye game,  anashauriwa aimbe Singeli kwa sababu tu labda ndiyo muziki unaobamba mtaani kwa sasa.
Kimsingi kuna wakati ushauri wa aina hii huwa ni ‘tango pori’, hauna manufaa kwa msanii na mara nyingi huwa ni chachu ya kupotea zaidi kwa msanii.
Hawawafahamu mashabiki wao
Unaposikia ‘mzee’ anaukandia muziki wa kina Alikiba na Diamond siyo kwamba anamaanisha hawajui kuimba, isipokuwa anajaribu kukufafanulia kwamba yeye binafsi anawapenda wasanii waliounogesha ujana wake kuzidi hawa wa sasa.
Ugumu kwa wasanii wanaotaka kurudi ni kwamba wanatumia nguvu kubwa kufanya muziki kwa ajili ya mashabiki wa kileo, wakati watu wanaoelewa na kuwapenda zaidi ni wale ambao waliwasikiliza kipindi kile wanabamba—hao ndiyo mashabiki wao.

Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...