» » Raia Marekani waendelea na maandamano kumpinga Trump

Raia Marekani waendelea na maandamano kumpinga Trump


Wengi wanasema dini isiwe sababu ya kubaguliwa
Image captionWengi wanasema dini isiwe sababu ya kubaguliwa
Raia nchini Marekani bado wanaendelea na maandamano ya kupinga amri ya kiutawala iliyotolewa na Rais Trump inayozuia kwa muda raia wanaotoka mataifa saba ya kiislamu kuingia nchini Marekani.
Hata hivyo, tangu hatua hiyo kutolewa, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa raia wa nchi mbalimbali huku baadhi wakiunga mkono hatua hiyo, na wengine wakiipinga vikali kwa kusema kuwa ni makosa watu kubaguliwa kutokana na imani zao za kidini.
Wakati huo huo, Kaimu mwanasheria mkuu nchini Marekani ameamuru idara ya wanasheria kutoitetea mahakamani amri hiyo.
Sally Yates, ambae aliteuliwa na Barack Obama, amesema bado hajashawishika kwamba inaruhusiwa kisheria.
Waandamanaji wanasema hatua hiyo ni kukiuka haki za binaadam
Image captionWaandamanaji wanasema hatua hiyo ni kukiuka haki za binaadam
Baadhi ya wanadiplomasia wa Marekani wameandika waraka unaopinga amri hiyo, ambapo wamesema katu haitaifanya Marekani kuwa salama.
Lakini msemaji wa Rais amewajibu kwa kuwaambia, wafuate amri hiyo au waondoke.
Nae aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama amevunja ukimya kwa kutoa taarifa inayosema amesikitishwa na maandamano yanayoendelea nchini humo.
Trump aliagiza kuzuia waislam wa nchi saba kuingia Marekani
Image captionTrump aliagiza kuzuia waislam wa nchi saba kuingia Marekani
Msemaji wa Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba Rais huyo mstaafu hakubaliani na fikra ya kubagua watu kutokana na imani zao za kidini.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...