» » Mkuu wa Mkoa Awashusha Vyeo Walimu Wakuu 63 Kisa Mkoa Kuwa wa Mwisho Kitaifa Matokeo ya Form Two

 
SIKU mbili baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kutangaza matokeo ya kidato cha pili na shule tisa za mkoa wa Mtwara kushika mkia, Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendegu ameagiza mamlaka husika kuwavua vyeo walimu wakuu wa shule za msingi 63 kutokana na matokeo hayo.

Akizungumza  juzi Dendegu alisema alichukua aumuzi huo baada ya kujiridhisha kutokana na utafiti ambao waliufanya baada ya matokeo ya darasa la saba yaliyotoka mwaka jana.

Alisema taarifa zilizopo zinaonesha wanafunzi hao wa kidato cha pili waliofeli walifanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba hali ambayo inaibua maswali mengi katika kufeli huko.

Mkuu huyo alisema zipo changamoto mbalimbali ambazo zipo pia katika mikoa mingine ila Mtwara zimekuwa zikitumiwa kama sababu za changamoto za mitihani.

“Hawa wanafunzi walifaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2014/15 hivyo ni jambo la kushangaza kuona leo wanafeli, lazima kuna uzembe kwa wasimamizi wa watoto hao katika ngazi ya msingi,” alisema.

Alisema baada ya kuhoji baadhi ya walimu, walidiriki kusema kuwa walitoa majibu kwa wanafunzi hao hali ambayo ilichangia ufaulu, hivyo kusababisha kilichotokea.

Mkuu wa Mkoa alisema pamoja na walimu wakuu hao kushushwa vyeo, bado wanaendelea na mkakati wa kubaini udhaifu wa walimu wa sekondari na pia maofisa elimu ili wajiandae kuwajibika.

Dendegu alisema zipo changamoto kama ufundishaji wa mazoea, kufanya mambo kwa kufupisha, utoro kwa wanafunzi, wazazi kukosa mwamko na zingine nyingi.

Alisema pamoja na changamoto hizo, wana mikakati ya kutoa chakula na kutaka maofisa elimu kufuatilia shule mbalimbali lakini bado uzembe upo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...