Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea taarifa na kukagua shughuli za mgodi huo. Alisema atamwagiza pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), apitie hesabu za kampuni hiyo tangu mwaka 2011 ilipoanza uzalishaji.
Ruvuma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuliza maswali mazito kuhusu mapato na matumizi ya kampuni ya makaa ya mawe ya Tancoal na papo hapo akaagiza uchunguzi wa haraka wa kijinai.
Majaliwa alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea taarifa na kukagua shughuli za mgodi huo. Alisema atamwagiza pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), apitie hesabu za kampuni hiyo tangu mwaka 2011 ilipoanza uzalishaji.
“Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” alisema.
Miongoni mwa maswali aliyouliza Waziri Mkuu, alitaka kujua ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambalo ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70) licha ya kuwa imekuwa ikizalisha makaa ya mawe na kuyasafirisha kwenye viwanda ndani na nje ya nchi.
“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 na mkauza zaidi ya hapo. Mkaguzi wa hesabu anasema kampuni imepata hasara, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Mlingi Mkucha.
Majaliwa auliza maswali mazito Tancoal
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment