KARIBU KATIKA KIPINDI CHA UUMBAJI
SURA YA PILI,
CHANZO CHA KIFO.
🔷JE,KIFO KILISABABISHWA NA NINI?????
Tunaendelea..............................
Maandiko yanaonesha kwamba Baada ya MUNGU kumuumba Adamu na kumuweka katika Bustani ya Edeni, alimpatia maagizo ambayo alipaswa kuyafuata.
📓Tunasoma hivi " Bwana MUNGU akamwagiza huyo Mtu akisema ,Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwamaana siku utakapo kulamatunda ya mti huo utakufa hakika." mwanzo 2:16-17.
👁👁Kwahiyo sharti la kuendelea kuishi lilikuwa kwamba Mwanadamu kumtii MUNGU kwa kutokula matunda ya mti walio katazwa.
BAADA YA HAPO KULITOKEA NINI?????
🚶Siku moja wakati Hawa akitembea bustanini, alijikuta amesimama chini ya mti uliojulikana kama mti wa ujuzi wa mema na mabaya,ambao walikatazwa kula matunda yake.
👁👁Wakati akiutizama mti huo na kuyastaajabia matunda yake, huenda maswali kadhaa yalikuwa yakipita akilini mwake.
🤔Akiwa katika kutafakari, ghafla alisikia sauti ikimsemesha. Sauti hiyo haikuwa MUNGU, wala ya mumewe, Adamu; ilikuwa ni sauti ya nyoka.
🐍Nyoka! Ndio, ilikuwa sauti ya nyoka. Je, kama angalikuwa wewe ungelifanyaje???????
je, umewahi kusemeshwa na kiumbe mwingine zaidi ya Binadamu??? na Je, ikitokea hivyo, utafanya nini??
📓Hebu maandiko yatuambie jinsi ilivyo kuwa "Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowaumba BWANA MUNGU. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyo sema MUNGU, Msile Matunda ya miti yote ya bustani??
mwanzo 3:1
👉Hivi ndivyo mazungumzo yao yalivyoanza.
Huenda kabla ya Hawa kujibu, kile kitendo cha nyoka kuongea kingetosha kumfanya Hawa ashtuke, na kukimbia mara moja kutoka eneo hilo na kumtafuta Mumewe,Adamu,ili aje aone kioja hiki cha nyoka kuongea kama wao,kwani tangu wameubwa;- walikuwa hawajawahi kisikia nyoka akiongea.
Lakini haikuwa hivyo, Hawa alijiamini na kudhani angeweza kukabiliana na jambo lolote na kushida, kwahiyo akaingia kwenye mjadala na nyoka.
🙇Tuendelee kusoma na kuona mazungumzo yao yalivyo kwenda aya ya 2-6 inasema,
"Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustani twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwamaana MUNGU anajua yakwamba siku mtakayo kula matunda ya mti huo, Mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama MUNGU, Mkijua mema na mabaya.
💃Mwanamke alipoona yakuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa ktk matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala"
😭Uasi dhidi ya amri ya MUNGU ukawa umetendeka.
DHAMBI IKAWA IMEINGIA KTK DUNIA YETU, na kufuatiwa na matokeo yake mabaya.
🙇👉Tangu hapo, ndani ya mwanadamu kumekuwa na nia ya kutaka kuwa mungu ( yaani, kuwa mwenye mamlaka yote juu ya maisha yake) na kuishi kama apendavyo mwenyewe na sio kuwa chini ya mamlaka ya mwingine.
👉Nia ya kutaka awe mtawala wa maisha yake na kutenda apendavyo yeye mwenyewe. Nia ya kutaka awe mkuu juu ya wengine kila inapowezekana. Nia ya kuwa juu au kujiinua juu ya MUNGU.
😭Lakini ktk kisa hiki cha anguko la Adamu na Hawa .........................
TUTAENDELEA KIPINDI KIJACHO....
Ili tuone baada ya hao kula tunda nini kilitokea
Somo hili limeandaliwa na;-
N.Malale.
kama unaswali,ushauri na maombi
usisite kunitafuta;-
0763 30 70 24,
nashmalale@yahoo.com
No comments:
Post a Comment