Stori: Imelda Mtema, Gazeti la Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: KITUKO! Wakati pongezi za kufa mtu zikielekezwa kwa muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kupata mtoto wa kiume kwa mchumba’ke, Chuchu Hans, muigizaji huyo ameibuka na kushangaa watu wanaoeneza habari za kujifungua kwa Chuchu wakati si kweli kama amejifungua.
Ray alitoa kioja hicho Alhamisi iliyopita wakati akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamozi baada ya kupigiwa simu ili kumpongeza kwa kupata baby boy.
Awali, taarifa za uhakika zililifikia gazeti hili Jumatano iliyopita kuwa Chuchu amejifungua salama mtoto wa kiume katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar.
Baada ya kujiridhisha kutoka kwa marafiki wa karibu na kinywa cha Chuchu mwenyewe na kukiri kuwa amejifungua salama mtoto huyo wa kiume, ndipo Risasi Jumamosi lilipompigia Ray bila kumueleza kwamba jana yake waliongea na mpenzi wake, mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kaka hongera kwa kupata baby boy.
Ray: Nani kasema mimi nimepata mtoto?
Risasi Jumamosi: Kaka mbona hilo lipo wazi kwamba umepata mtoto wa kiume na sisi tumejiridhisha kwa mtu wa karibu na ‘baby’ wako Chuchu.
Ray: Huyo mtu atakuwa ana matatizo, sijapata mtoto. Nifiche ya nini?
Risasi Jumamosi: Mbona unaonekana kuchenga wakati hili ni jambo la kheri?
Ray: Kaka mimi ndiyo nakuambia ukweli, najua ni jambo la kheri sasa kwa nini nifiche? Mimi nashangaa tu hii mitandao kusema nimepata mtoto sijui Chuchu kajifungua, sijui hizo habari wanazitoa wapi.
Risasi Jumamosi: Kaka kuna sababu gani ya kuficha wakati hata Chuchu mwenyewe amekiri?
Ray: Kama amesema hivyo atakuwa ana matatizo naye. Mimi sizijui hizo habari. Na huo ndiyo ukweli wangu.
Ray alikinzana na mpenzi wake Chuchu ambaye alikiri hivi alipozungumza na mwanahabari wetu siku alipojifungua:
“Daah ila namshukuru Mungu sana kwa kila jambo na ni mwema kwangu.”
MHARIRI
Kupata mtoto ni jambo la kheri hivyo Ray hakuwa na sababu ya kuficha. Yawezekana hakujua kama mwanahabari wetu amewasiliana na mchumba’ke na kujiridhisha lakini hata hivyo hakuna kilichoharibika. Tunakupongeza Ray na tunakushauri uwe tu muwazi katika mambo haya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment