Kwa Picha: Maisha ya Fidel Castro
Picha za maisha ya Amri jeshi mkuu Fidel Castro,aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti na kuiongoza Cuba kwa miaka 50
- Fidel Castro alizaliwa mwaka wa 1926, mkoa wa kaskazini mashariki wa oriente nchini Cuba na tajiri wa ukuzaji wa miwa. Alijiunga na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo.
- Baada ya miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi yaliyotibuka, alienda mafichoni nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi kikaongoza. Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe 1, mwaka 1959, kama waziri mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista.
- Mwaka 1961, Castro aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya wapiganaji raia wa Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni waliokuwa wanafadhiliwa na CIA na waliovamia Bay of Pigs kupigana dhidi ya serikali yake. Aliwashinda.
- Alipata majaribio kubwa mwaka 1962, pale rais wa Marekani John Kennedy alipoionya Urusi kuondoa makombora yake kutoka Cuba.
- Mwishowe, viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa.
- Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa besiboli. Hapa anaonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa 1962.
- Baadhi ya raia wa Cuba walimchukulia kama dikteta kwa kuwakandamiza wapinzani.
- Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao ,kuelekea Marekani, kwa kutumia maboti yaliyokuwa hatari.
- Lakini Fidel Castro alipata uungwaji mkono, na kuwa miongoni mwa viongozi waliohudumu kwa miaka mingi duniani
- Baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya urais kakake Raul. Alioneka mara chache hadharani, kabla ya kung’atuka madarakani mwezi Februari mwaka 2008.
- Mwezi Septemba mwaka 2015, Fidel Castrol alihutubia umma kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne. Hotuba yake ilikuwa ya kwanza tangu mwezi Julai mwaka 2010 alipotoka kufanyiwa upasuaji wa utumbo. Alionekana kwa umma alipokuwa akisherehekea mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwake mwezi Agosti.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment