» »Unlabelled » 🔥🔥 *HATARI YA KUWA NA MAHUSIANO YA UCHUMBA NA ZAIDI YA MTU MMOJA*

🔥🔥 *HATARI YA KUWA NA MAHUSIANO YA UCHUMBA NA ZAIDI YA MTU MMOJA*🔥🔥
 
💧Miongoni mwa utapeli unaofanyika makanisani na vijana, ni kuchumbi au kuchumbiwa na watu zaidi ya mmoja na wote unawapa matumaini Ya kuwaoa au kuolewa nao
💧Huo ni utapeli, uhuni  na upagani ulokomaa.
💧Hii ni dalili kuwa hujiamini na hufai kuaminiwa katika sekta ya mahusiano na ndoa
💧Hii ni dalili kuwa hukumuomba Mungu wala kumuhusisha katika suala lako la kumpata mwenzi wa maisha, badala yake unavamia tu.
💧Hiyo ni ishara ya namna gani huna maarifa hata kidogo katika sekta ya mahusiano na ndoa (hisia na mapenzi)
💧Hiyo ni ishara ya namna gani usivyo mwaminifu na huwezi kuwa mwaminifu ktk ndoa
💧Hiyo  ni ishara ya jinsi ulivyo na roho ya Kuto ridhika na hutoridhika kwa huyo utakaye mpata
🙅🏻Acha Utapeli wa Mapenzi Jipange upya
😫 *NINI KITAKUKUMBA  KWA KUWA NA MAHUSIANO ZAIDI YA MOJA* 😫
👹Utakuwa na roho ya Kuto ridhika ktk ndoa
👹Siku mkihitirafiana na mwenzako katika ndoa utamkumbuka yule ulo mpiga chini utahisi angekuwa afadhali kuliko huyu
👹Utaoa/kuolewa na ambaye hukukusudia kumuoa /kuolewa naye
👹Utakuwa mtu wa kumkosoa mwenzako kila mara, kwa kumlinganisha na mchumba ulo mpiga chini
👹Utapata tatizo la kisaikolojia katika ndoa yako, ambalo halifutika
🙅🏻Acha kujitengenezea matatizo makubwa ya baadaye yatakayo kugharimu maishani mwako
🙅🏻 *ACHA UTAPELI WA MAPENZI*🙅🏻
👉🏻Binti Kama humpendi kijana, acha kumtumainisha kwa kumwonyesha upendo wa kisanii ili akusindikize kabla ya wewe kupata umpendaye ili usiwe mpweke.
👉🏻Binti usipokee zawadi yeyote kutoka kwa kijana kama humpendi na huna mpango naye wa kuoana naye.
👉🏻Binti usijifanye maarufu wa kukataa vijana na kuwa piga vibuti, siku wakikoma kukufuata, utawafuata kwa machozi.
👉🏻Kijana, usifanye haraka kumwambia binti nataka nikuoe, kama hujajihakikisha kuwa huyu ndiye hata aje wa viwango zaidi ya huyu sibadiri msimamo.
👉🏻Kijana, usifanye haraka kutoa zawadi nyingi na kubwa kwa binti kama hamja fika ngazi ya juu ya uchumba (kulipa mahali) siku ukipigwa kibuti utazimia, na usimdai ulivyo mpa
👉🏻Kijana /binti usipende kusema uongo na kuficha hali yako na ya familia yako kisa utaachwa, usijifanye matawi kumbe mizizi, utakuja kuumbuka.
👉🏻Usipende kuazima vitu kama nguo, usafiri, mawasiliano, pesa ili mwenzako akuone uko vizuri, onyesha uhalisia wako, akupende kama ulivyo
👉🏻Usipende kuumiza watu hisia zao, kupiga vibuti ipo siku Mungu atayageuza kwako itakuuma vibaya.
👉🏻Usimdharau mtu kwa hali unayomuona nayo kwa mara ya kwanza anapo elezea feelings zake kwako, hujui baadaye atakuwa na maisha gani, Wewe siyo Mungu upange maisha, mkatae mtu kwa sababu Mungu hajakupa kibali moyoni juu yake.
           Somo hilu ni refu sana ili nimejitahidi sana kurisummarize hope utapata kitu.
Mungu akubariki na kukuonekania.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...