» »Unlabelled » Vijana wakwamisha Uchaguzi DRC

Vijana wakwamisha Uchaguzi DRC


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Image captionRais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ametupilia mbali shutuma kwamba amesogeza mbele tarehe ya uchaguzi ili aendelee kung'ang'ania madarakani.
Amesema serikali yake isingependa kuacha idadi kubwa ya wananchi wake na wengi wao wakiwa ni vijana ambao hawakujiandikisha kupiga kura na wakose haki yao ya kupiga kura .
Mwishoni mwa wiki iliyopita,kiongozi wa tume ya uchaguzi nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo alitangaza uwezekano wa kusogezwa tarehe ya kupiga kura hadi hapo desemba 2018.
Moja ya maandamano Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Image captionMoja ya maandamano Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Siku za hivi karibuni Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo imekuwa ikikumbwa na maandamano ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakilenga ucheleweshwaji wa uchaguzi nchini humo.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles