» »Unlabelled » Mji wa Kinshasa wabaki kama mahame DRC

Mji wa Kinshasa wabaki kama mahame DRC


Kinshasa
Biashara zimefungwa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na hakuna magari barabarani kufuatia wito wa upinzani kwa watu wakae ndani katika kushinikiza uchaguzi mkuu nchini ufanyike Novemba na Rais Kabila ajiuzulu.
Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya usalama vimeizingira nyumba ya mpinzani mkuu wa rais Kabila, Etienne Tshisekedi, ambye ndiye anayongoza wito wa uchaguzi ufanyike Novemba mwaka huu.
Chama chake kimeonya kuwa rais Kabila atakuwa anatekeleza 'uhaini wa hali ya juu' iwapo uchaguzi utacheleweshwa.
Etienne TshisekediImage copyrightREUTERS
Image captionEtienne Tshisekedi
Katiba inamzuia Kabila kuwania muhula wa tatu, na upinzani unatuhumu kuwa serikali inataka kuchelewesha uhaguzi huo ili Kabila asalie madarakani.
Chama tawala na kimoja cha upinzani vimependekeza kuchelewesha uchaguzi wa urais hadi Aprili 2018.
Kinshasa
Kinshasa
Tume ya uchaguzi inasema inahitaji muda zaidi kuweka sawa orodha ya wapiga kura.
Watu kadhaa wameuawa Kinshasa mwezi uliopita katika maandamano ya kumtaka rais Kabila aondoke madarakani Desemba.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles