» »Unlabelled » Trump na Clinton wapambana tena katika mdahalo

Trump na Clinton wapambana tena katika mdahalo


wagombea Urais Marekani katika mdahaloImage copyrightAFP
Image captionwagombea Urais Marekani katika mdahalo
Wagombea Urais nchini Marekani Donald Trump na Hilary Clinton wamechuana tena katika awamu ya tatu na ya mwisho ya mdahalo mjini Las Vegas, ikiwa zimebaki siku chache tu, kufanyika uchaguzi nchini humo.
Wamepambana vikali katika masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa silaha, utoaji mimba na uhamiaji haramu.
Na moja kati ya eneo waliovutana ni kuhusu uhusiano kati Marekani na Urusi na silaha za nyuklia.
Wakati Donald Trump akionyesha kuna haja ya uhusiano na Urusi na rais Vladmir Putin, Hillary Clinton anaona Urusi ni hatari kwa Marekani na hata kutupiana maneno makali.
Kuhusu umiliki wa Silaha mgombea urais wa Democratic amesisitizia msimamo wake kuhusu sheria kali katika umiliki wa silaha.
Kwa upande wake Donald Trump alimshutumu Bibi Clinton kwamba amejinufaisha kwa fedha zisizo halali.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles