» »Unlabelled » Fundisho la leo kwa jamii yetu

Fundisho la leo kwa jamii yetu

Mara nyingi tunapoingia kwenye Maduka Makubwa (Supermarkets or Shopping malls) tunalipa Bei Ileile iliyobandikwa Kwenye bidhaa husika. Yani kama simu imebandikwa Mil.2 unalipa bila kuuliza mara mbili. Wakati mwingine unaweza kukuta bidhaa ambayo unajua bei yake lakini ukiikuta Supermarket unalipa tu kama hujui bei.

Kwa mfamo unaweza kukuta nguo unafahamu bei yake ni elfu 20 lakini ukiikuta Mlimani city inauzwa elfu 50 huuliza wala huombi kupunguziwa bei. Unalipa kama ilivyo hata kama unajua kuwa unaibiwa. Unaogopa usionekane mshamba, na unahofia hata ukibargain hutapunguziwa.

Lakini Cha Ajabu Tunapopita Magengeni Kununua mahitaji madogo ya nyumbani kama Ndizi, nyanya, vitunguu, samaki etc mchezo Wetu Wa Kuomba Kupunguziwa Bei (Bargaining) Hauna Kipimo. Yani ndizi inauzwa Sh.200 lakini unalazimisha uuziwe kwa Sh.100.

Hebu tafakari Mjane Masikini Mwenye Watoto watano Wanaomtegemea anakwambia Ndizi Moja Ni Sh.200 lakini bado unamlazimishe akupunguzie. Anajaribu Kukueleza Ni Jinsi Gani ilivokuwa Ngumu Kununua Hizo Ndizi, anakueleza anavyoamka saa 9 usiku ili saa 11 alfajiri awe Kariakoo kununua hayo mahitaji aje kuuza.

Anakueleza Jinsi Gani Hali Ya Maisha Ilivo Ngumu Saivi, na mwisho kabisa anakueleza yeye ni mjane. Mumewe alifariki na kumuachia mzigo wa watoto watano awalee na kuwasomesha. Anafika mbali na kukueleza anaishi na wanae chumba kimoja cha kupanga na anategemea biashara hiyo kulipia kodi, kusomesha watoto, kula, kuvaa, matibabu etc. Kwa kifupi biashara hiyo ni maisha yake.

Lakini pamoja na maelezo yote hayo bado unalazimisha, '' Usiponiuzia sinunui'', Na Kwa Jeuri unajifanya Kuondoka. Lakini Kwa Kuwa Kwa mjane huyu Nusu Ya Mkate Ni Afadhali Kuliko kukosa kabisa, analazimika Kukuita Na Kukuuzia Kwa Bei uliyoitaka wewe ambayo wakati mwingine haina Faida Kabisa.

Wewe unaondoka kwa kufurahia umepata mahitaji kwa bei chee lakini mwenzako Moyoni analia. Umemuacha na majonzi. Ana Wasiwasi Ni Jinsi Gani Ataweza Kuishi wa Wanawe. Kimyakimya Anajipa Moyo, anaamini ipo Siku Mungu atamfungulia Njia.

Hebu Chukua Mda Kidogo Tafakari Kuhusu Hili. Tusipende KuBargain Sana Na Watu Kama Hawa. Wanafanya Hizo Biashara Sio Kwa Ajili Ya Kujenga majumba makubwa, au kununua Magari Ya Kifahari Bali Ni Kwa Ajili Ya Kuishi Na Kulisha Watoto Wao.!

Share kama imekugusa.!!

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles