» »Unlabelled » Rais wa Zambia aapishwa kwa muhula mwingine

Rais wa Zambia aapishwa kwa muhula mwingine


Lungu alipata asilimia 50.35 ya kura zilizopigwa
Image captionLungu alipata asilimia 50.35 ya kura zilizopigwa
Rais wa Zambia Edga Lungu ameapishwa hii leo baada ya kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya upinzani kushindwa katika kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Lungu
Image captionMwandishi wa BBC anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Lungu
Mahakama ya katiba ilitupilia mbali kesi ikisema kuwa upinzai ulikuwa umeishiwa muda wa kupeleka suala hilo mahakamani.
Bwana Lungu alishinda uchaguzi wa tarehe 11 mwezi Agosti kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichokwa kuepuka kurudiwa tena kwa uchaguzi.
Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema alishindwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mahakamani
Image captionMgombea wa upinzani Hakainde Hichilema alishindwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mahakamani
Hakainde Hichilema ambaye alichukua nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye uwanja wa National Heroes katika mji mku wa Zambia Lusaka, anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Edga Lungu.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO KARIBU TENA

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles