» »Unlabelled » Ndege za kivita za Marekani zapaa Korea

Ndege za kivita za Marekani zapaa Korea


Ndege za jeshi la Marekani aina ya B-1B zikipaa juu ya Pyeongtaek, Korea Kusini 13 Septemba, 2016.Image copyrightREUTERS
Image captionNdege za jeshi la Marekani aina ya B-1B zikipaa juu ya Pyeongtaek, Korea Kusini 13 Septemba, 2016.
Ndege mbili za kivita za Marekani zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia, B-1 Lancer, zimepaa juu ya anga ya Korea Kusini, siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la tano la silaha za nyuklia.
Ndege hizo zilipaa si mbali sana kutoka ardhini juu ya kituo cha kijeshi kinachopatikana kilomita 77 kutoka mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.
Marekani imeitahadharisha Korea Kaskazini kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taifa hilo baada ya kufanyika kwa majaribio hayo ya bomu Ijumaa.
Jaribio hilo la Pyongyang ndilo kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na taifa hilo.
'Ndege aina ya B-1 zina uwezo wa kubeba makombora yenye mabomu ya nyuklia au mabomu ya nyuklia yenyewe yenye uwezo wa kuharibu hata mahandaki.
Vincent BrooksImage copyrightREUTERS
Image captionKamanda wa jeshi la Marekani eneo la Korea Jenerali Vincent Brooks (pili kutoka kulia) amesema hatua ya Pyongyang imezidisha hali ya wasiwasi eneo hilo
Operesheni hiyo ya kupaa kwa ndege ilikuwa imepangiwa kufanyika Jumatatu lakini ikacheleweshwa kutokana na hali mbaya ya hewa Guam, eneo ambalo ndege hizo hukaa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO KARIBU TENA

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles