Rais Kenyatta atangaza vita dhidi ya uvuvi haramu
FRIDAY , 2ND SEP , 2016
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameviagiza vyombo vya dola kufanya doria katika bahari ya India ili kudhibiti uvuvi haramu ambao umekuwa ukiathiri uchumi wa mkoa wa Pwani na taifa zima kwa ujumla.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Akiongea wakati wa kufungua maonesho ya Mombasa ASK, Rais Uhuru amesema licha ya Kenya kuwa na hazina kubwa ya samaki katika eneo la Bahari ya Hindi hainufaiki chochote kutokana na uvuvi haramu.
Amesema kuwa watu wa Kenya wanahitaji ajira wakati sekta ya uvuvi ikihujumiwa na mataifa mengine, hivyo basi ni lazima uvuvi haramu usitishwe ili kuwawezesha vijana wa Kenya kufanya uvuvi ili kuboresha uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment