 |
Pichani ni Miili ya Watu 15 waliofariki na wengine 203 kujeruhiwa katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufuatia tetememko la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya ritcher 5.7 lililotokea mkoani humo ikiwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo kunafanyika ibada ya kuaga miili hiyo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aungana na Wanabukoba katika Ibada hiyo leo Septemba 11,2016.
|
 |
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro amesema bado Kamati ya Ulinzi na Usalama ikishirikiana na vikosi vya uokoaji pamoja na majeshi la ulinzi na usalama vinaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa majengo na mali uliosababishwa na Tetemeko hilo.
Mhe. Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitaendeleo kutolewa kadri zitakavyopatikana kutokana na kuendelea kwa kazi ya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.
|
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO
KARIBU TENA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment