» »Unlabelled » Gazeti la Nation Mirror lililoandika makala ya rushwa lafungiwa Sudan Kusini

Gazeti la Nation Mirror lililoandika makala ya rushwa lafungiwa Sudan Kusini


Rais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu wanashutumiwa kujilimbikizia mali wakati raia wakiteseka na vita
Image captionRais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu wanashutumiwa kujilimbikizia mali wakati raia wakiteseka na vita
Mhariri wa gazeti linaloongoza Sudani Kusini amesema serikali imeamuru kufungwa kwa gazeti hilo, siku moja baada ya kuchapisha makala ya madai ya rushwa kwa maafisa wa ngazi za juu.
Siku ya jumanne gazeti la Nation Mirror lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari kuhusu ripoti ya waangalizi wa Marekani ambayo inamshtumu Rais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu kujilimbikizia mali wakati raia wa kawaida Sudan kusini wakihaha na hali mbaya ya maisha.
Mhariri wa gazeti hilo Aurelious Simon Chopee amesema kuwa hakuna taarifa yoyote rasmi aliyopewa juu ya kufungwa kwa gazeti hilo.
Na hakuna taarifa yoyote ile kutoka mamlaka ya nchi.
Serikali ya Sudan Kusini imekuwa ikikosolewa kwa kuwaekea vikwazo waandishi wa habari.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO KARIBU TENA

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles