» »Unlabelled » Bosco Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa wiki mbili ICC

Bosco Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa wiki mbili ICC


Mshirikishe mwenzako
Bosco NtagandaImage copyrightAFP
Image captionKiongozi wa zamani wa waasi DRC anakabiliwa na mashtaka 18
Aliyekuwa kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Bosco Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa takriban wiki mbili katika kizuizi chake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhaini huko Hague, Shirika la AFP linaripoti..
Anakakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita.
Amepewa jina la utani "The Terminator" kutokana na shughuli zake Congo, Ntaganda aligoma kula kulalamika dhidi ya hali inayomkabili kizuizini, ikiwemo kuhusu suala la kutembelewa na familia yake.
AFP imemnukuu wakili wake Stephane Bourgon aliyesema kwamba ameanza tena kula.
Ameongeza:
''Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, mkewe atafika The Hague kuanzia Alhamisi na ataweza kumuona bwana Ntaganda kwa kiwango fulani cha faragha, kitakachokidhi matarajio yake."
Mwaka jana, Ntaganda alikana mashtaka 18 yanayomkabili - ikiwemo mauaji, kuwasijili watoto katika jeshi na kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles