» »Unlabelled » Watu sita wafariki kutokana na tetemeko la ardhi Italia

Watu sita wafariki kutokana na tetemeko la ardhi Italia


Tetemeko la ardhi ItaliaImage copyrightREUTERS
Image captionMajumba mengi yameporoka katika miji iliyo eneo la Umbria
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter limetikisa eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukua watu chini ya vifusi, maafisa wa Italia wamesema.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.
Mitetemeko ilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma na Italia. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica.
Watu wanne wameripotiwa kufariki katika eneo la Accumoli, na meya wa mji jirani wa Pescara del Tronto amesema watu wawili wazee walifariki baada ya nyumba yao kuporomoka.
Eneo hilo, ambalo linapakana na mikoa ya Lazio na Marche, ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia.
Tetemeko la ardhi
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia la ulinzi wa nchi hiyo.
Meya wa mji wa Amatrice Sergio Perozzi ameambia kituo cha redio cha serikali cha RAI kwamba mji huo umeharibiwa vibaya.
"Barabara za kuingia na kutoka mjini hazipitiki. Nusu ya mji imeharibiwa. Watu wamefukiwa chini ya vifusi… kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja moja ambalo huenda likaporomoka," amesema.
Shirika la kulinda raia Italia limeeleza tetemeko hilo kuwa "mbaya".
Tetemeko la ardhiImage copyrightREUTERS
Tetemeko hilo awali lilikisiwa kuwa la ukubwa wa 6.4. Lilifuatwa na mitetemeko mingine mikubwa, gazeti la
La Repubblica limeripoti.
USGS wamesema uharibifu huenda ukawa mkubwa.
Mwaka 2009, tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 lilitokea eneo la Aquila, na kusikika pia katika mji wa Roma. Watu zaidi ya 300 walifariki.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...