Thailand kuruhusu jeshi kuendelea kutawala
Wapiga kura nchini Thailand wameidhinisha katiba mpya ambayo itaruhusu jeshi kuendelea kuongoza taifa ilo.
Kampeni zote za kupinga uamuzi huo zikiwa zimezuiliwa na serikali ya kijeshi pasipo kutoa ufafanuzi wa kutosha.
Matokeo ya kura zilizopigwa yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura wanaunga mkono mabadiliko ya katiba. Huku asilimia hiyohiyo ndiyo itakayohusika kumchagua waziri mkuu.
Nchi ya Thailand inaongozwa kijeshi baada ya kufanya mapinduzi miaka miwili iliyopita. Jeshi linaamini kuwa katiba mpya itaimarisha nchi hiyo kufuatia misukosuko ya kisiasa iliodumu kwa takribani miaka kumi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment