» »Unlabelled » MWENGE WATINGA NYAMAGANA UKITOKEA MISUNGWI

MWENGE WATINGA NYAMAGANA UKITOKEA MISUNGWI


Mwenge wa uhuru ukiingia katika Wilaya ya Nyamagana ukitokea Wilaya ya Misungwi. Hapa ni makamanda wa mwege wakionyesha umahiri wao katika ukimbizaji wa Mwenge.

Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Captain Honest Ernest Mwanossa akitoa hotuba ya Mwenge leo katika viwanja vya shule ya Buhongwa mara tu baada ya kuwasili Wilaya ya Nyamagana ukitokea Wilaya ya Misungwi leo.

Mkuu wa Wilaya Misungwi Mhe. Lugaila akisoma risala ya kukabidhi Mwenge kwa Mkuu wa wilaya wa Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga.

Gwaride la skauti.

Heshima.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mama Lugaila.

Saluti kwa Ahlah.

Saluti kwa Ahlah Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mama Lugaila akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na Mwenge wa Uhuru.

Shule ya Sekondari Buhongwa na yo ni kati ya miradi iliyozinduliwa leo na Kiongozi wa kitaifa wa Mwenge Captain Honest Ernest Mwanossa  katika mbio za mwenge wilayani Nyamagana.

Buhongwa Saccos moja kati ya miradi iliyozinduliwa leo kwenye mbio za Mwenge katika wilaya wa Nyamagana. 

Mbio za Mwenge wa uhuru leo asubuhi zimewasili katika wilaya ya Nyamagana zikitokea Wilaya ya Misungwi ambapo umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Misungwi.

Akizungumza na wananchi walijitokeza leo kuupokea mwenge wa uhuru, Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Kitaifa Captain Honest Ernest Mwanossa amesema kuwa kauli mbiu ya mwenge mwaka huu ni wananchi washiriki katika sensa ya kitaifa ili wahesabiwe na pia wajitokeze kutoa maoni kuhusu marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga, Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mhe. Lugaila amesema kuwa mwenge wa uhuru umezindua miradi mingi ya maendeleo na kuwasihi watendaji wa miradi iliyozinduliwa kufanya kazi kwa bidii ili kulinda heshima ya Mwenge na rasilmali ya Serikali.
Akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga amesema kuwa mwenge wa mwaka huu katika wilaya ya Nyamagana atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya zaidi ya shilingi bilioni nne.
Moja kati ya miradi iliyozinduliwa leo ni shule ya sekondari Buhongwa na chama cha akiba na mikopo Buhongwa Saccos na Mwenge huo ukutarajiwa kuzindua miradi mingine katika wilaya ya Nyamagana kabla ya kukabidhiwa kwa wilaya ya Sengerema kesho asubuhi.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...