MWENGE WATINGA NYAMAGANA UKITOKEA MISUNGWI
Mwenge wa uhuru ukiingia katika Wilaya ya Nyamagana ukitokea Wilaya ya Misungwi. Hapa ni makamanda wa mwege wakionyesha umahiri wao katika ukimbizaji wa Mwenge. |
Mkuu wa Wilaya Misungwi Mhe. Lugaila akisoma risala ya kukabidhi Mwenge kwa Mkuu wa wilaya wa Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga. |
Gwaride la skauti. |
Heshima. |
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mama Lugaila. |
Saluti kwa Ahlah. |
Saluti kwa Ahlah Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mama Lugaila akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga. |
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na Mwenge wa Uhuru. |
Shule ya Sekondari Buhongwa na yo ni kati ya miradi iliyozinduliwa leo na Kiongozi wa kitaifa wa Mwenge Captain Honest Ernest Mwanossa katika mbio za mwenge wilayani Nyamagana. |
Buhongwa Saccos moja kati ya miradi iliyozinduliwa leo kwenye mbio za Mwenge katika wilaya wa Nyamagana. |
Mbio za Mwenge wa uhuru leo asubuhi zimewasili katika wilaya ya Nyamagana zikitokea Wilaya ya Misungwi ambapo umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Misungwi.
|
Akizungumza na wananchi walijitokeza leo kuupokea mwenge wa uhuru, Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Kitaifa Captain Honest Ernest Mwanossa amesema kuwa kauli mbiu ya mwenge mwaka huu ni wananchi washiriki katika sensa ya kitaifa ili wahesabiwe na pia wajitokeze kutoa maoni kuhusu marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga, Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mhe. Lugaila amesema kuwa mwenge wa uhuru umezindua miradi mingi ya maendeleo na kuwasihi watendaji wa miradi iliyozinduliwa kufanya kazi kwa bidii ili kulinda heshima ya Mwenge na rasilmali ya Serikali.
Akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga amesema kuwa mwenge wa mwaka huu katika wilaya ya Nyamagana atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya zaidi ya shilingi bilioni nne.
Moja kati ya miradi iliyozinduliwa leo ni shule ya sekondari Buhongwa na chama cha akiba na mikopo Buhongwa Saccos na Mwenge huo ukutarajiwa kuzindua miradi mingine katika wilaya ya Nyamagana kabla ya kukabidhiwa kwa wilaya ya Sengerema kesho asubuhi.
Tupe maoni yako
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment