» »Unlabelled » Mwanasheria Mkuu wa Serikali Avitaka vyama vya siasa kuheshimu tamko la polisi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Avitaka vyama vya siasa kuheshimu tamko la polisi


Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aonya vyama vya siasa kutumia maneno yanayovunja amani na usalama wa nchi.

Masaju ambaye amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, ametolea mfano Oparesheni UKUTA iliyotangazwa kufanywa na CHADEMA na kusema kuwa ina maneno ya kijeshi yanayotumiwa kwenye shughuli za kihalifu.

Amesema neno UDIKTETA siyo sahihi kwa kuwa nchini Tanzania hakuna udikteta kwa kuwa serikali inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na nchi inaendeshwa kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka wa katika miimili yote mitatu ya dola.

“UKUTA lengo lake ni nini, ni sawa na kuwatenganisha wananchi na serikali yao” Amesema Masaju na kuwataka wananchi kutambua kuwa Septemba Mosi ni siku ya Majeshi nchini huku akishangazwa na CHADEMA kuchagua siku hiyo kuzindua kampeni yao aliyodai kuwa ina lengo la kuvuruga nchi.

Masaju amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kutii mamlaka za dola ikiwemo Jeshi la Polisi na mahakama iliyowapa mwongozo juu ya ombi la kupinga zuio la jeshi la polisi na pia kufuata ushauri waliopewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora juu ya kutokuwepo kwa udikteta nchini.

Amesema sababu kuu za kuzuia Oparesheni ni mbili ambazo ni hali ya usalama kutokuwa shwari, pamoja na kutokuwepo kwa udikteta nchini.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...