Italia: Ibada yafanyika kwa ajili ya waliokufa katika tetemeko la ardhi
Ibada ya wafu imefanyika nchini Italia kwa ajili ya watu 290 waliofariki dunia katika tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatano wiki hii.
Siku ya kitaifa ya maombolezi imeanza nchini Italia, kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko kubwa la ardhi, lilokumba maeneo ya katikati mwa taifa hilo.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amehudhuria mazishi ya mazishi ya kitaifa ya waliofariki dunia katika eneo lililopata pigo kubwa, Arquata.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika maeneo yaliyoathirika.
Zaidi ya watu 280 wanaaminika kwamba wameaga dunia.
Takriban watu 400 kwa sasa wanatibiwa hospitalini.
Matumaini ya kupata watu wakiwa hai kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa yanafifia baada ya siku tatu za uokoaji.
Raia wengi wa Italia waliaga dunia, pamoja na raia kadhaa wa kigeni.
Bendera ya taifa hilo inapeperushwa nusu mlingoti.
Zaidi ya watu 200 waliuwawa katika eneo la Amatrice pekee.
Watu 2,000 wameachwa bila makao.
Tetemeko la ardhi lilikuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter, lilitokea mapema jumatano, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Italia Roma.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment