» »Unlabelled » Afrika Kusini ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika

Afrika Kusini ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika


sarafu ya nairaImage copyrightAFP
Image captionMabadiliko yametokana na kushuka kwa thamani ya naira dhidi ya dola
Afrika kusini ndiyo yenye uchumi mkubwa Afrika .Kwa miaka mwili iliyopita, Nigeria ilidai kuwa kileleni, lakini mahesabu mapya ya matumizi ya viwango vya sarafu yameliweka taifa la Afrika Kusini tena kileleni.
Mahesabu mapya yanazingatia kiwango vya shirika la fedha la kimataifa(IMF) vya tarakimu za pato la jumla la ndani ya nchi kwa nchi zote mbili katika mwaka 2015.
Katika kipindi cha mwaka huu kufikia sasa, randi ya Afrika kusini na naira ya Nigeria zimekua na mwelekeo tofauti dhidi ya dola. Thamani ya randi iliongezeka kwa takriban asilimia 16%, huku naira ikipoteza robo ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani.
Lakini hakuna cha mno sana - kwani kwa dola bilioni 301 Afrika kusini imeipiku Nigeria kwa dola bilioni 5 tu.
Uchumi wa mataifa hayo mawili uko katika hatari ya kuanguka katika msuko suko kutokana na kwamba uchumi wa mataifa haya mawili ulididimia katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...