Kufanya Biashara katika Intaneti:
Biashara 5 za Kuanza Nazo Bure
UKIFA MASKINI NIUCHAGUZI WAKO MWENYEWE
Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za
kufanya biashara aidha kwa kuuza huduma au bidhaa. Lakini wachache sana hasa
Afrika ambao wanafikiria kufanya biashara katika intaneti. Kuna mbinu nyingi
tofauti za kufanya biashara katika intaneti ambazo zinatoa fursa kwa
wajasiriamali kujiongezea kipato.
Kinachohitajika ni simu au kompyuta yenye kuunganishwa na
mtandao wa intaneti na pia kuwa umejiunga na mitandao ya kijamii ,au mmiliki wa
tovuti au blogu (ambazo unaweza kupata bure) au barua pepe.
Zifuatazo ni baadhi ya programu zinazokuwezesha kupata fedha
kupitia intaneti:
1. Kuuza Bidhaa Za
Biashara Yako Kupitia Tovuti
Unaonesha biadhaa zako na bei,wanunuaji wanaziona na kuweka oda
ya manunuzi. Wanalipa kwa Kadi ya Benki Credit /Debit Card) na fedha inaingia
katika akaunti yako benki. Au kwa kutumia malipo kwa mfumo wa simu kama M-Pesa
,Tigo Pesa na Airtel Money kwa Tanzania.
2. Kuuza Bidhaa Za Biashara Ya Watu Wengine Kupitia Tovuti
Unajisajili na baadhi ya makampuni yanayouza bidhaa mtandaoni
duniani kama Amazon na eBay na kisha kuonesha bidhaa
zao katika tovuti au blogu au katika mitandao ya kijamii kama facebook na
twitter. kisha watu wakinunua bidhaa hizi kupitia matangazo yako basi unapata
kiasi cha malipo waliyofanya yaani kamisheni.
Kujiunga fuata linki:
§ Amazon
§ eBay
3. Kuuza Matangazo Kupitia Tovuti Au Blogu
Kuna makampuni mbalimbali dunia ambayo yana wakutanisha
watangazaji na wauzaji kupitia matangazo katika tovuti au blogu.
Watangazaji wanajiunga nakutuma matangazo ya biashara yao na
wauzaji wenye tovuti wanajiunga nakuruhusu matangazo kuonekana katika tovuti
zao.
Wauzaji wa matangazo wanalipwa kila tangazo linapoonekana katika
tovuti au watu wanapo bonyeza matangazo haya.
Unahitaji kuwa na tovuti au blog ili kufanikiwa katika programu
hii.
4. Kufanya Kazi Za Ajira Kupitia Mtandao
Kuna makampuni ambayo yanataka wafanyakazi katika mtandao ambao
wanaweza kufanya kazi fulani na wanalipwa wakikamilisha.
Baadhi ya kazi ni kama kutengeneza tovuti, kutengeneza programu
za komputa au simu, kuchapa,kusikiliza na kutohoa suuti kwenda maandishi n.k
Badhi ya mitandao inyotoa huduma hizi ni surveycompare.net , odesk.com,onlinejobs.net ,elance.com , peopleperhour.com na fiverr.com
5. Kutangaza Biashara Kwa Kutuma Linki
Mbinu hii ndiyo hasa ninayopenda kuisisitiza hapa. Sababu ya
kusisitiza nimkwasababu inafanya kazi kwa haraka na urahisi. Huhitaji kuwa na
tovuti wala blogu kufanikisha. Kama tu upo katika mitandao ya kijamii kama
facebook,twitter,intagram na mingine kama skype,whatsapp na pia kwa email
unaweza kufanikiwa sana kwa kutuma linki ambayo marafiki zako wakiifungua
utapata malipo.
Mfano Nimesoma katika intaneti kitu kizuri juu ya kupunguza
unene na nataka marafiki zangu wanene wafidike kama haupo katika bishara hii
nitatuma linki katika kundi katika facebook mfano na sitapata chochote.
Lakini ukiwa katika programu hizi unawezeshwa wewe kupata malipo
kila unapofanya hivyo. Rahisi
Kama una marafiki wengi basi uwezo wako wa kufanikiwa ni mkubwa
sana
Ifuatayo ni mitandao inayotoa huduma hii:
a
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment