👣Hiki ni kisukari wanachopata wanawake wakati wanapokuwa wajawazito .
👣Baadhi ya wanawake wanakuwa na viwango vikubwa sana vya glucose katika damu zao na miili yao haina uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha kuweza kusafirisha glucose hiyo hadi kwenye seli za miili yao hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika miili yao.
👣Kisukari hiki huweza kudhibitiwa vizuri kwa kula chakula kinachofaa na kufanya mazoezi , Ni asilimia ndogo kati yao ambao huhitaji kupewa dawa. 👣 Gestational diabetes isipodhibitiwa huweza kusababisha matatizo wakati wa uzazi au kufanya mtoto anayezaliwa kuwa mkubwa kuliko alivyostahili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment