» » Imani yenye Maarifa na utashi

MWANGAZA (UTASHI)-Glow tracts by Kibidula Farm
Yoel na Marko walikuwa marafiki wawili waliokuwa na imani tofauti kabisa. Yoeli alimwamini Mungu kama Mfalme Mweza yote, Aliyeumba kila kitu ulimwenguni. Marko alikuwa mtu asiyeamini kabisa juu ya MUNGU, aliyedhihaki dini na kufikiri kuwa dunia yote-pamoja na yeye mwenyewe-vilitokana na ajali. “Unajuaje Kuwa MUNGu yupo na Biblia sio tu kitabu chenye visa vya uongo?” Mara kwa mara Marko alipinga. “Mungu yupo kwa sababu Biblia inasema hivy na unaweza kuiamini Biblia kwasababu ni Neno la MUNGU,” Yoeli angemjibu hivyo. Kisha Marko angemcheka kuhusu hilo na kusema, “Hivyo ni sawa na kusema, ' Mimi ni mtendakazi bora kwa sababu Frank amesema hivyo. Je, unaweza kumwamini Frank? Kwasababu nasema tunaweza kumwamini.” Mantiki ya mzunguko iliyotolewa na Yoeli ina makosa na haitamshawishi mtu yeyote kuhusu uwepo wa MUNGu au kwamba Biblia ni Kweli. Hata hivyo bado wengi leo hawana sababu nzuri zaidi ya hapo kwaajili ya imani yao katika Biblia. Je, kuna ushahidi wowote wa kweli unaothibithisha kuwa Biblia ni  kweli? Je, maarifa na mantiki hutoweka pale watu wanapokuwa Wakristo?
Ndoto
(2)Njia mojawapo ya kupima usahihi wa Biblia ni kuungalia utabiri wake. Moja ya madai ya Mungi ni kwamba YEYE, kupitia Biblia, anaweza kuelezea mambo ya wakati ujao (Isaya 46:9,10). Kwa kuchunguza kumbukumbu za kihistoria za Babeli ya kale katika kitabu cha Danieli kunatusaidia kujibu swali kuhusu usahihi wa Biblia. Hapa tunamwona mfalme anayeitwa Nebukadneza, mtawala ambaye habari zake zimeandikwa si tu katika Biblia, lakina pia katika kumbukumbu za kihistoria zingine
(1) Usiku mmoja aliota ndoto muhimu sana. Hata hivyo, alipoamka, hakuweza kuikumbuka ile ndoto-ila tu ilimsumbua. Aliwaita wenye hekima wake na kuwaamuru wamwelezee ndoto yake na tafsiri yake. Wenye hekima hao walistaajabishwa na ombi lake, wakasema, “Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme...”   (Danieli 2:10), Mfalme akaghadhabika sana akaamuru kwamba wenyewe hekima wote wa Babeli wauwawe (Danieli 2:12). Hapa ndipo Mwebrania mmoja aitwaye Danieli anapoingia kwenye kisa hiki. Danieli alikuwa amechukuliwa kama Mateka kwenda Babeli alipokuwa kijana mdogo tu. Danieli alikuwa akimwamini Mungu. Wakati Arioko, mkuu wa kikosi cha walinzi wa mfalme alipomwambia Danieli kuhusu amri ya mfalme, Danieli alikwenda kwa Mfalme na kumwomba ampatie muda ili aweze kumweleza ndoto yake na tafsiri yake, Mfalme akakubali.  Danieli akaenda nyumbani na kwa moyo wa dhati akamwomba Mungu ili ampatie hekima. Mungu akajibu maombi yake, na, “Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku” (Danieli 2:19).

SANAMU KUBWA YA KIHISTORIA
Asubuhi iliyofuata Daniel Akaenda kwa mfalme na kumfunulia ile ndoto. Mfalme alikuwa ameona sanamu kubw. Ilikuwa na sehemu kuu tano tofauti. 
Kichwa kilikuwa cha dhahabu.
Kifua chake na mikono yake ilikuwa ya fedha
Tumbo lake na viuno vyake vya shamba
Miguu yake ni ya chuma
Na nyayo za miguuyake ilikuwa nusu ya chuma na nusu ya udongo
Kisha jiwe kubwa likaipiga ile sanamu na kuiseta vipande vipande, vikama kama makapi, nao upepo ukavipeperusha (Danieli 2:31-35) Ndipo Danieli akamwambia Mfalme maana ya ile ndoto. 
Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha ufalme wa Babeli (Danieli 2:38)
Fedha iliwakilisha Uyunani
Miguu ya chuma iliwakilisha Urumi
Miguu ya chuma iliyochanganyika na udongo iliwakilisha utawala wa Rumi uliogawanyika, nusu yake ukiwa na nguvu na nusu dhaifu. Kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyika na udongo, mataifa haya yasingeweza kuungana pamoja. Lile jiwe kubwa lililoipondaponda ile sanamu iliwakilisha  ufalme wa Mungu. “Na.... Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hatuaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali atavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele”  (Danieli 2:38-44)

KUTIMIA kwa NDOTO
Kila mmoja ya utabiri wa falme zilizowakilishwa na madini mbali mbali zilitimia kwa usahihi kabisa. 
Ufalme wa kwanza, Babeli uliitawala dunia tangu mwaka 605 hadi 539KK
Taifa la Waamedi na Waajemi lilitawala tangu 539-331KK. 
Utawala uliofuatia, Uyunani, ulitawala kuanzia mwakak 331-168KK
Dola ya Rumi iliyowakilishwa na chuma ilitawala tangu mwaka         168-476KK
Ufalme wa mwisho, uliogawanyika katika falme ndogondogo nyingi, huwakilisha utawala wa Rumi iliyogawanyika, ambayo  ni mataifa ya Ulaya kwa sasa, ambayo bado sahihi katika utambuzi wake wa falme zote tano na muda ambao zingeanza kutawala 
Mfano Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, 
USHAHIDI MUHIMU ZAIDI
Watu wanaoshuku wamependekeza kuwa utabiri wa Danieli wa uongo, kitabu chake kimeandikwa baadaye zaidi katika historia. Hata kama hii ingekuwa sahihi, ukliwe kuwa “Magombo ya Bahari ya Chumvi” Yana Machapisho nane kutoka katika kitabu cha Danieli, Chapisho la zamani kabisa hukadiriwa kuwa la mwaka 125KK
(3)(Ambalo lenyewe pia ni nakala ya chapisho la awali zaid) Huonesha kuwa unabii huu uliandikwa miaka mia moja kabla ya Rumi haijagawanyika kuwa mataifa ya Ulaya ya sasa. Unabii huu ni mfano mmoja tu kati ya mia inayoweza kuoneshwa ili kuthibithisha kuwa Biblia imevuviwa na MUNGU. Mfano mwingine mzuri unaonekana katika unabii wa Danieli sura ya tisa ambapo utimilifu sahihi wa ubatizo na kifo cha Kristo vilitabiriwa mamia ya miaka kabla ya matukio hayo
(4)Na hakika kwlei, baada ya kuchunguza ushahidi kama tulionao kwenye uanbii wa Biblia, tunaweza kufikia uamuzi kuwa tunaweza kumwamini MUNGU na kuiamini Biblia! Sura ya Pili ya Danieli hutuonesha jinsi ambavyo mojawapo ya unabii mbalimbali wa Biblia ulivyo wa kweli na sahihi, jambo linalotupatia msingi wa kuwa na imani yenye maarifa. Biblia ni Neno la MUNGU lililovuviwa na inaweza kuaminiwa kama mwongozo wetu katika KILA  jambo.
Hata hivyo, kuiamini tu habari hii kutaifanya tu iwe hivyo-habari. Kitendo cha kuiamini peke yake hakina nguvu ya kuyaokoa maisha yetu. Lazima tubadilishwe kwa njia ya imani yetu katika ile kweli. Ni jambo lenye umuhimu wa milele siyo tu katika kuiamini Biblia, lakinai kuiruhusu itubadilishe pia. Biblia inasema kwamba “Mashetani nao wanaamini na kutetemeka!”  Yakobo2:19. Mungu atayachukua maisha yetu na kuyabadilisha kuwa kitu fulani chema ikiwa tutamruhusu. Je tunamruhusu?
1.Tafuta mtandaoni, katika Wikipedia “NebuchanezzarII”
2.“The Next Super Power”-Mark Finley
3.“Maana ya Dead Sea Scrolls” uk 137. James C Vanderkam.          Peter Flin

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...