» » KAINI ALIMUOA NANI?

 
KAINI ALIMUOA NANI?
Kaini alikuwa ni mtoto wa kwanza MWANZO 4:1 “1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.”, akifuatiwa na ndugu zake Habili na Sethi MWANZO 4:2,25 “2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili…. 25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi...” Hawa walikuwa ni kizazi cha kwanza, ingawa watoto waliotajwa ni watatu tu, Adamu alikuwa na watoto wengine wake na waume MWANZO 5:4 “4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.” . Mwanahistoria wa Kiyahudi aliandika kuwa kama walivyosema wazee wa kale Adamu alikuwa na watoto 56, wa kiume 33 na wa kike 23. Biblia haituambii walikuwa watoto wangapi lakini kwa kuangalia umri wa maisha ya Adamu miaka 930 tunakubaliana kuwa walikuwa ni watoto wengi. MWANZO 5:5 “5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.”
Kumbuka kuwa Adamu na Hawa waliambiwa wazae wakaongezeke MWANZO 1:28 “28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi….”
Adamu alimzaa Sethi akiwa na miaka 130 akaishi miaka 800 mingine ndipo akafa (MWANZO 5:4).Mwanamke aliambiwa atazidishiwa uchungu MWANZO 3:16 “16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
JE! KAINI ALIMUOA NANI?
»Kuna madai kuwa Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili alitoka na kwenda Nodi na ndiko alikompata mwanamke/mke wake (MWANZO 4:17) na kusema kuwa kipindi hicho Nodi ilikuwa na watu walioishi tangu zamani (pre adamic human/pre adamiam)kabla ya Adamu kuwepo na kudai kuwa aliyeolewa na Kaini ni moja ya watu hao(Pre adamic human / pre adamism). Wengine husema alikuwa ni moja ya malaika walioasi.
»Biblia iko wazi sana kuwa mtu wa kwanza ni Adamu(MWANZO 1:26), Adamu anaitwa mtu wa kwanza  ( 1 WAKORINTHO 15:45). Kabla ya Adamu kuumbwa hakukuwa na mtu duniani(MWANZO 2:5-8) Mungu alipomuumba Adamu akaona yuko peke yake, Mungu akamfanyia wanyama na ndege lakini hawakufanana naye (MWANZO 2:18-20) ndipo akamfanyia Hawa"Eve" yaani mama wa viumbe vyote (MWANZO 3:20).
Hivyo ni vyema tukatambua kuwa hao watu wanaodaiwa kuwepo " pre adamic humans" hawakuwepo kwa sababu hata kabla Mungu kuumba dunia inaoneaha hakukuwa na watu (MWANZO 1:1-2).
Ukisoma katika MWANZO 6:1-2 “1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” Hawa wanaoitwa wana wa Mungu ni Malaika walioasi wakatupwa hapa duniani ndipo wakawapenda binti za wanadamu wakawaoa maana yake ni kwamba hao Malaika walikuwa ni wa kiume, kwa hiyo kwa sababu hii bado inagoma kusema kuwa Kaini alioa moja ya malaika hawa kwa sababu wao walikuwa ni wa kiume. Sababu ya pili inayodhihirisha kuwa hakuoa miongoni mwa malaika hawa ni kwamba hawa walikuja kuonekana miaka mingi kupita ambapo tayari ulimwengu ukiwa na watu wengi ambapo tayari Kaini alikuwa ameshaoa miaka mingi sana iliyopita.
»Tunaposoma neno " MKE" kwa lugha ya kiebrania ni "ishshah"  linamaanisha WOMAN/ WIFE /FEMALE yaani MWANAMKE/MKE. Mwanamke ni yule aliyetokana na Adamu MWANZO 2:23 “23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.”
»Kumbe tunaona kuwa Kaini Hakuna pre adamic human / pre adamism bali alioa mwanamke aliyetokana na Adamu mwenyewe.
»Hivyo nasi, bila shaka Kaini alimuoa dada yake au mtoto wa ndugu yake.
Zamani ilikuwa si kosa kaka na dada kuoana. Abraham alimuoa dada yake, Sara (MWANZO 20:12), Amramu, baba yake Musa alimuoa shangazi yake(KUTOKA 6:20), Yakobo alioa binti za mjomba wake (MWANZO 29:1-35). Miaka 400 baadaye Mungu akabadili utaratibu, akazuia dada na kaka kuona (MAMBO YA WALAWI 18:6-18).
»NOTE: Biblia inaposema " akamjua MKE" haimaanishi "akaoa" bali ni kushiriki tendo la ndoa MWANZO 4:17 “17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko...” .  Mariamu alikuwa hajamjua mume lakini tayari alikuwa ameposwa na Yusufu LUKA 1:34 “34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?”
»Hivyo basi , Kaini alipoondoka kuelekea Nodi alikuwa na MKE wake na alipoondoka aliwaacha ndugu wengine wengi waliotaka kumpiga baada ya yeye kumuua Habili.
MWANZO 4:15 “15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.”
NAAMINI UNABARIKIWA SANA NA MASOMO HAYA.
NI MIMI Ev. Zachary John Bequeker
MWANZA – TANZANIA
+2557585904890 /+255 625966236
Kwa mafundisho Zaidi tembelea
www.zakachekainjili.blogspot.com

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...