Baba Askofu Kakobe amesema kuwa mahojiano hayo yaligusa moja kwa moja kuhusu uraia wake ambapo amehojiwa maswali mengi kuthibitisha kama ukweli askofu huyo wa kiroho ni raia wa Tanzania, mbali na mahojiano hayo amesema kuwa idara hiyo imefanikiwa kuchukua hati zake nne anazotumia kusafiria, kwa ajili ya kuthibitisha baadhi ya taarifa zinazopatikana katika hati hizo.
Aidha amesema kuwa idara hiyo imejiridhisha kuwa yeye ni raia wa Tanzania.
Katika mazungumzo yake amelinganisha tukio hilo na maandiko katika biblia katika Mithali 28:1
”Muovu anakimbia hata kama hajafuatwa na mtu, lakini mwenye haki ni jasiri kama simba”, hivyo amesema yeye ni jasiri kwani hana hatia yeyote.
Amesema ”Mimi sina uovu wowote mimi ni raia wa nchi hii, kwahiyo nimetoa maelezo yote ya kina kwamba mimi ni raia wa hapa” amesema Baba Askofu Kakobe.
Lakini pia amegusia kuwa utafiti juu ya uraia wake umeanza kufuatiliwa muda mrefu ambapo kuna watu wamekuwa wakitumwa kijijini kwao kuthibitisha uraia wake na kukuta hana hatia yoyote.
"Mimi nilijiunga na jeshi la kujenga taifa mwaka 1974 mpaka sasa ni miaka 44 nimeenda kuwa trained kama mwanajeshi maana yake hiyo, miaka 44 imepita leo sasa ndiyo wananza kuzungumza masuala ya uraia unaona kabisa kuna shida, hivyo ni rahisi mtu kudhani kuna jambo, kwanini sasa?
" Pamoja na kazi nzuri hii ambayo ni kazi yao na kawaida yao lakini ni rahisi kuhisi kitu kingine. Sasa hivi wamechukua passport yangu na wamesema sababu ya kuchukua passport hiyo ni kwamba kule itakuwa rahisi kupata taarifa za 'Afidavit', ambazo zinatakiwa kwenye maelezo.
"Na nimetoa taarifa za passport zangu nne kwa sababu nimekuwa na passport nne katika kipindi chote na nimetoa kila kitu kuhusu passport hizo" alisema BabaKakobe
Baba Askofu Kakobe ameongezea kuwa bado hajafahamu sababu za idara hiyo kufuatilia uraia wake.
Tembelea www.Zakachekainjili.blogspot.com kwa Neno la Mungu.
By Zachary John Bequeker, +255 625966236
Download App YETU hapa⬇⬇
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment