» » Waziri Kalemani Awapo ONYO Watumishi TANESCO

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewatangazia kiama wafanyakazi wa TANESCO nchini watakaoshirikiana na watu kuiba miundo mbinu ya umeme, ili kuhakikisha huduma hiyo haihujumiwi kama zingine.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na maafisa wa TANESCO, na kusema shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa kufuatia umeme unaopotea, kutokana na kuhujumiwa miundo mbinu yake, na wizi wa umeme uliokithiri unaofanywa na baadhi ya wateja.

Taarifa hiyo imetolewa  baada ya TANESCO kugundua wateja zaidi ya mia moja wanatumia umeme bila kulipia hali inayolitia hasara shirika, baada ya kufanya operesheni maalum ya kukagua watu wanaoiba umeme jijini Dar es salaam.

Kufuatia operesheni hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakiyakimbia makazi yao kuogopa kutiwa mikononi mwa polisi, na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles