» » Zitto Kabwe: Huu sio Utanzania ni umafia.....Usiku Kucha Sijalala Namuwaza Lissu

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa, anaeleza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

“Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu,” amesema Zitto katika taarifa aliyoitoa leo Ijumaa.

Lissu alijeruhiwa kwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.

Mbunge wa Singida Mashariki, Lissu alisafirishwa jana usiku baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Zitto amesema, “Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama nchi, kama Taifa.”

Amesema kilichotokea kwa Lissu jana Alhamisi ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana na utamaduni wa ustahimilivu na udugu ambao nchi imekuwa ikisimamia.

“Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia,” amesema.

Amesema Watanzania wanaolitakia mema Taifa wana kila sababu ya kulaani na kukataa utamaduni wa kimafia kuzoeleka nchini.

“Tusimame kulaani kwani #HuuSiUtanzania,” amehitimisha Zitto katika taarifa yake.
 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...