» »Unlabelled » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 51
Tulipoishia, Chaajabu alikuwa hata hageuki kuniangalia. Nikajua hapa kuna namna lakini nikasema mpaka nimuue hata kama nitakamatwa. Nilimfuata mpaka nilipomkaribia na kuinua kisu kumchoma ghafla_____Songa nayo......Kuna kundi la watu wasiopungua watano walitokeza na kunikamata. Kisha wakanidhibiti vizuri sana na nikaanza kupokea kipigo kutoka kwao bila kikomo kisha wakampisha Zabroni ambapo naye akaanza kunipiga kwa sifa haswaa. Niliumia sana hasa pale niliposikia leo tunakuua kidudu mtu wewe unakatisha mambo ya watu mjini hapa mwehu wewe.
Kipigo kiliendelea mpaka ilifika wakati nikalegea kupindukia. Zaboni aliingiza mkono mfukoni na kuchomoa sindano fulani kisha akaiweka dawa akitaka kunichoma. Ghafla kuna polisi walitokeza eneo lile na kuanza mashambulizi. Hali ile iliwafanya Zabroni na kundi lake kukimbia mbio. Hapo ndipo nikatelekezwa pale na polisi wakaja kuniokoa. Wakati wananipandisha kwenye difenda japo nilikuwa na maumivu makali lakini kuna kitu nilikiona na sikuamini macho yangu kwa kile ninachokiona. Niliona kama Peris ndiye alikuwa na kile kikosi cha jeshi la polisi. Nilishangaa kiasi lakini ilionyesha yeye alikwa na pikipiki yake na akaamua kutokomea mimi nisimwone. Sikujali sana.
Baada ya kufika kituoni nilipokelewa na kukimbizwa hospitalini. Nilipewa matibabu hospitalini chini ya usimamizi wa jeshi la polisi. Kisha baada ya mda na mimi kupata nafuu nilishangaa polisi wote wameondoka na kisha madaktari wakaja na kusema umeruhusiwa. Mmh nilishangaa kiasi kwani nilijua nitakamatwa. Pili nilijuwa nitalipishwa pesa ya matibabu lakini sikudaiwa hata kidogo hali ile ilinifanya niende kwa mhasibu nitafute jina la mtu aliyenilipia matibabu ni nani? Niliinuka na kutafuta ofisi ya mhasibu kwa pale hospitalini kisha nikaipata na nikaingia ndani.
Mara baada ya kusalimiana naye nilimweleza shida yangu. Hakuwa mgumu ambapo aliangalia orodha ya malipo yaliyofamywa siku ile kisha akaniuliza kwni vipi? Nikamjibu hapana nahitaji tuu kujua aliyenisaidia. Ndipo akanionyesha daftari kuangalia jina liliandikwa lingine. Lakini mwandiko na sahihi vilikuwa ni vya Peris. Nilikuwa nimeshapata majibu kuwa Peris ndiye alinilipia. Nikamshukuru mhasibu kisha nikaondoka zangu. Nilitembea kuelekea kwenye maficho yangu yale ya pili. Nilifika na kuingia ndani nikalala. Asubuhi kulivokucha nikaanza kutafakari jinsi ya kumaliza swala lile kwani tayari lilianza kuonekana linanishinda.
Niliumiza sana kichwa lakini majibu sikupata. Mara nikiwa nimekaa pale simu yangu ikaita. Ilikuwa ni namba ngeni nilisita kiasi kuipokea baadae nikaamua kuipokea ndipo nikasikia sauti ya baba. Hujambo Yuu? Mimi baba yako niko......... Mara simu ikakatika. Nilipiga ikawa haipatikani nilipiga mara nyingi lakini haikupatikana kabsa. Nilichekecha akili ya haraka nikaona suluhu niwahi ofisi za mawasiliano hizi za mitandao kisha waniambie ile namba inasoma emeo gani. Niliingia chumbani nikavaa nguo safi kabsa safari ya kuelekea huko ikaiva.
Nilitembea nikahisi nachelewa nikachukua bodaboda mpaka ofisi fulani iko pale Mwananyamala. Walinipokea na kunihudumia kisha wakanionyesha mahali ile namba inadoma. Pia wakaniambia inaonekana ile namba hua haitumiki mara kwa mara. Zaidi wakaniambia inaonekana huyu mtu huwa anawasiliana na kiongozi wa ngazi ya juu ya Jeshi la wanachi kwani ujumbe wingi uliokutwa ni kutoka namba ya huyo kiongozi. Kisha wakaniambia kuwa huyu mtu inaonyesha huyu unaedai ni baba yako alisaidiwa na yeye kwani kuna baadhi ya ujumbe unaonyesha alikuwa akiwasiliana na yule kiongozi wa jeshi na kumwambia kuwa tayari nimemwokoa niko naye nyumbani kwangu Mbezi.
Yalikuwa maelezo niliyokuwa napewa na mhudumu yaani injinia wa mawasiliano katika kampuni kubwa sana hapa Tanzania. Alinieleza yale yote kutokana kuwa nilimweleza kila kitu mpaka kufikia pale. Pia nilimwonyesha kitambulisho ya kuwa mimi ni Afisa wa jeshi la polisi tena afisa mpelelezi. Basi akanielekeza jinsi ya kufika eneo ambalo line ile ilionyesha ndipo baba aliongelea na simu pia akanipa namba yake na kuniambia nikifika nimtafute atanielekeza nyumba.
Nilimshukuru sana kisha nikaanza safari ya kuelekea Mbezi. Nilitembea mpaka barabarani niliamua niende kwanza nyumbani kisha nitaelekea huko. Nilipofika nyumbani hata sikusumbuka nikafanya kilichonipeleka kisha nikapanda gari kuelekea Mbezi. Nilifika Mbezi mahali nilipoelekezwa kisha nikaanza kutafuta nyumba fulani za mitaa ile. Hapo nikafika nyumba moja na nilipoangalia ramani ilionyesha nimefika ndipo nikaamua kumpigia simu yule njinia.
Nilipopiga simu nikabiwa haipatikani. Nililaumu sana ile hali. Lakini ghafla akanipigia yeye. Nikapokea Nikamsikia akisema eeedh afande iho namba sasahivi inaonyesha iko hewai hebu piga. Nikamwambia sawa lakini pia niko Mbezi tayari nashindwa kujua ni nyumba ipi. Akanijibu hebu subiri kidogo nikuangalie wewe usawa wako. Baada ya dakika moja akasema hapohapo ulipo ndipo penyewe sasa hebu ingia nyumba "inayokuface" Kwa mbele. Nikamjibu sawa mkuu. Kisha nikakata simu.
Baada ya kukata simu niliipiga ile namba na kuambiwa inatumika. Hapo ndipo nikaamua kuingia kwenye lile jumba na kuanza kutembea mle ndani. Ghafla nikavamiwa na mijibwa mikubwa iliyoshiba mitatu. Ilikuwa mikubwa haswaa. Nilianza kwa kularuriwa nguo kisha mmoja akaanza kwa kunicharanga miguuni. Niliangushwa chini kisha nikawa nang'atwa sehemu mbalimbali. Mara ikasikika sauti kama ya Peris ikisema_____________________________________________________
____________________________________________________________
_______________________________________________Tukutane sehemu ya 52 tupate majibu. Naapenda woteeeeeee.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...