» » Nape Nnauye aeleza alichoambiwa na Tundu Lissu wakitoka bungeni jana

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisi mchana wakati wakitoka bungeni huku wakicheka.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe ni watuhumiwa, hama CCM mjomba.”

Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu akipelekwa Kenya alisema ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Ndege iliyomsafirisha iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita na robo usiku.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...