» » Mfumuko wa bei washuka nchini


Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa kipindi cha Julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwapo mwezi Juni mwaka huu hali inayomaanishakasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa imepungua.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa kipindi cha Julai mwaka huu kumechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2017 ikilinganishwa na bei za Juni 2016.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama, kwa asilimia 16.6, bilinganya (10.6), vitunguu (13.2), karoti (16.9) na viazi mviringo (13.5)" amesema.

Aidha ameeleza kuwa Shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma ulifikia Shilingi 91 na senti 87 kipindi cha Julai 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na senti 66 ilivyokuwa Juni 2017.

“Mfumuko wa bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya mfumuko huo wa Julai 2017 umepungua hadi asilimia 7.47 kutoka asilimia 9.21 Juni 2017 na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 5.70 kwa kipindi cha Julai kutoka asilimia 6.4 Juni 2017" ameongeza

Hata hivyo Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei wa kitaifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles