» » Mahakama Yatoa ONYO la Mwisho kwa Tundu Lissu


Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo.

Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani.

Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Ntobesya amedai kuwa mteja wake ana udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika.

Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo  ameahirisha kesi hiyo hadi August 14/2017.

Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles