» » Urusi; Putin aagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Urusi

US embassy in Moscow

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKufukuzwa wa wanadiplomasia hao kutapunguza idadi hadi 455
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.
Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo
Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.
Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.
US embassy dacha, Serebryany Bor, 28 Jul 17Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUrusi imewapiga wanadiplomasia wa Marekani
Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.
Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.
Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.
Warehouse used by US embassy in Moscow, 28 Jul 17Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUrusi inalitwaa ghala hili la Marekani lililo Moscow



Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...