» » Uhispania; Mtandao wa biashara ya ukahaba wavunjwa


Image captionBaadhi ya watu waliowahi kufungwa kutokana na kujihusisha na Mtandao wa biashara haramu za binadamu

Polisi nchini Uhispania wamesema wanawake 13 waliokuwa wamelazimishwa kufanya kazi za ukahaba katika kituo kimoja cha utalii mjini Puerto Banus wameachiliwa huru.

Wanawake hao wanadhaniwa kuwa waliletwa katika eneo hilo, kutoka nchini Bulgaria.

Polisi katika nchi zote mbili wamewakamata watu 34, wanaotuhumiwa kuwatishia wanawake hao na familia zao kuwafanyia fujo iwapo watakataaa kufanya kazi hiyo.

Kukamatwa kwa watu hao, kumekuja takriban miaka mitatu baada ya polisi kutahadharishwa kuhusiana na mtandao wa Ukahaba na wanawake ambaye alikwepa mtego wa kuingizwa katika biashara hiyo.

Polisi wanasema wanawake hao pia wamekuwa wakitumika kuibia wateja wake hao na kwamba baadhi yao walikuwa wakitumia madawa ya kulevya.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles